Jumamosi 17 Oktoba 2026 - 13:50
Sherehe za Kuzaliwa Bibi Zainab (s.a.)/ Waumini Wahimizwa Kuimarisha Hijabu, Heshima na Maadili

Hawza/ Jumuiya ya AhlulBayt ya Kenya imeungana na Hawza ya Sayyida Zainab (s.a.), iliyopo Kirigiti, Kaunti ya Kiambu, katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Bibi Zainab (s.a.), katika hafla iliyofanyika Ijumaa, tarehe 16 Oktoba 2026, sawa na tarehe 5 Jamadul Ula 1448 A.H., baada ya Swala ya Ijumaa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hafla hiyo ya kiroho na kimalezi ilipambwa na mihadhara yenye mafunzo muhimu pamoja na qaswida nzuri zilizowasilishwa na wanafunzi wa Hawza, kwa lengo la kueleza utukufu wa Bibi Zainab (s.a.), ambaye anajulikana kwa imani yake thabiti, subira, ujasiri na msimamo wake katika kutetea haki na kusimamia maadili ya Kiislamu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh Khamis Said, Mkurugenzi wa Hawza hiyo, alisisitiza umuhimu wa kujisitiri na kuzingatia mwenendo mwema, huku akibainisha kuwa maisha ya Bibi Zainab (s.a.) ni mfano bora unaopaswa kuigwa na wanawake wa Kiislamu katika kuhifadhi heshima, utu na maadili yao.

Kwa upande wake, Sheikh Juma Shughuli, Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya AhlulBayt ya Kenya, aliwahimiza wanafunzi kuiga mwenendo wa Bibi Zainab (s.a.) kwa kuzingatia hijabu inayotakiwa katika Uislamu, kudumisha heshima na hadhi yao, kuzingatia maadili mema na kushikamana kwa dhati na imani yao.

Aidha, hafla hiyo ilitoa fursa muhimu kwa washiriki kutafakari namna ambavyo maisha ya Bibi Zainab (s.a.) yanavyoweza kuwa mwongozo kwenye kizazi cha sasa, hususan katika malezi ya kiroho, ujenzi wa tabia njema na kuimarisha misingi ya maadili ya Kiislamu katika jamii. Ujumbe uliotolewa uliwahimiza wanafunzi na waumini kwa ujumla kuyafanya mafundisho hayo kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Sherehe za Kuzaliwa Bibi Zainab (s.a.)/ Waumini Wahimizwa Kuimarisha Hijabu, Heshima na Maadili

Sherehe za Kuzaliwa Bibi Zainab (s.a.)/ Waumini Wahimizwa Kuimarisha Hijabu, Heshima na Maadili

Sherehe za Kuzaliwa Bibi Zainab (s.a.)/ Waumini Wahimizwa Kuimarisha Hijabu, Heshima na Maadili

Sherehe za Kuzaliwa Bibi Zainab (s.a.)/ Waumini Wahimizwa Kuimarisha Hijabu, Heshima na Maadili

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha