Jumatatu 21 Septemba 2026 - 16:30
Mara'ji’ na Wanazuoni Wamtembelea Nyumbani kwa Ayatullah al-Udhma Shubayri Zanjani (ra) + Picha

Hawza/ Ayatullah al-Udhma Subhani, kundi la wanazuoni na shakhsia mashuhuri, viongozi wa Hawzah na viongozi wa mkoa, pamoja na makundi mbalimbali ya wananchi, walifika katika nyumba ya Ayatullah Shubayri Zanjani (ra) na kutoa salamu za rambirambi kwa mnasaba wa kufariki dunia Marji’ huyo wa Taqliid.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatullah Subhani, miongoni mwa Marjo’ wakuu wa Taqliid, alifika katika nyumba ya marehemu Ayatullah al-Udhma Shubayri Zanjani (ra), na kutoa salamu za rambirambi kwa mnasaba wa kufariki dunia Marji’ huyo wa Taqliid.

Ayatullah Arafi, Mkurugenzi wa Hawzah nchini Iran, pamoja na Ayatullah Husayni Bushehri, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom, pia walifika katika nyumba ya marehemu Hadhrat Ayatullah Shubayri Zanjani.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Muhammadi Araqi, Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Qom, pia alifika katika nyumba ya Marji’ huyo aliyefariki dunia, Hadhrat Ayatullah Shubayri Zanjani, na kutoa salamu za rambirambi kwa mnasaba wa kufariki kwake.

Wawakilishi wa nyumba za Mara'ji’ wakuu wa Taqliid, baadhi ya shakhsia za Hawzah, wajumbe wa Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Elimu ya Qom, Baraza Kuu la Hawzah na Bunge la Wataalamu wa Uongozi, pia walifika katika nyumba ya Marji’ huyo aliyefariki dunia.

Gavana wa Qom, viongozi wa mkoa na makundi mbalimbali ya wananchi pia walifika katika nyumba ya Hadhrat Ayatullah Shubayri Zanjani (ra), na kutoa salamu za rambirambi kwa mnasaba wa kufariki dunia Marji’ huyo wa Taqliid.

Mara'ji’ na Wanazuoni Wamtembelea Nyumbani kwa Ayatullah al-Udhma Shubayri Zanjani (ra) + Picha

Mara'ji’ na Wanazuoni Wamtembelea Nyumbani kwa Ayatullah al-Udhma Shubayri Zanjani (ra) + Picha

Mara'ji’ na Wanazuoni Wamtembelea Nyumbani kwa Ayatullah al-Udhma Shubayri Zanjani (ra) + Picha

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha