Jumatatu 21 Septemba 2026 - 16:45
Marji’ Aliyefikia Kilele cha Maadili na Fiqhi

Hawza/ Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom, huku ikitoa salamu za rambirambi kufuatia kufariki dunia Ayatullah al-Udhma Shubayri Zanjani, imesisitiza kwamba: Faqihi huyo mchamungu alikuwa amefikia kilele cha juu katika nafasi ya kielimu na kimaadili, pamoja na sifa na ukamilifu wa nafsi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ujumbe kamili wa rambirambi wa Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom kufuatia kufariki dunia Ayatullah al-Udhma Shubayri Zanjani, mmoja wa Mara'ji’ wakuu wa Taqliid, ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake tutarejea.

Imam Swadiq (as) amesema:

«إذا ماتَ المُؤمِنُ الفَقیه ثُلِمَ فی الإِسلامِ ثُلمَةٌ لا یَسُدُّها شَیء»

“Anapofariki dunia muumini faqihi, ufa hutokea katika Uislamu ambao hakuna kitu kinachoweza kuuziba.”

Kufariki dunia Marji’ mwenye cheo cha juu wa Mashia, Hadhrat Ayatullah al-Udhma Hajj Sayyid Musa Shubayri Zanjani (Mwenyezi Mungu amrehemu), kumeleta masikitiko na huzuni kubwa.

Faqihi huyo mchamungu alikuwa amefikia kilele cha juu katika nafasi za kielimu na kimaadili, pamoja na sifa na ukamilifu wa nafsi, na kiti chake cha kufundishia kilikuwa miongoni mwa viti vya masomo vilivyokuwa na maudhui mengi na kuvutia sana kwa wanafunzi wa elimu za Kiislamu.

Wanazuoni wengi wenye fadhila walinufaika kutokana na ujuzi mpana ya kielimu na kimaadili wa Marji’ huyo mkuu, na hadi vizazi vijavyo, watafutaji elimu na Fiqhi wataendelea kunywa kutoka chemchemi ya fadhila zake.

Mwalimu huyo mnyenyekevu, mwenye zuhdi na aliyeishi maisha ya kawaida, alikuwa wa kipekee katika uwezo wake wa kufanya ijtihadi, uelewa wake mpana wa Fiqhi na kauli za mafaqihi, pamoja na nguvu na umakini wake katika Fiqhi. Katika elimu ya Rijal, alikuwa miongoni mwa wanazuoni mashuhuri na bora zaidi wa zama hizi.

Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom inatoa salamu za rambirambi kwa mnasaba wa msiba huu mkubwa kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi (Mwenyezi Mungu aendelee kuhifadhi utukufu wake), Mara'ja’ wakuu wa Taqliid (Mwenyezi Mungu aendelee kuwalinda), Hawzah, taifa tukufu la Iran, hususan wananchi waheshimiwa wa Qom ambao kwa miaka mingi walinufaika na hali ya kiroho ya Swala ya Jamaa yake katika Haram ya Hadhrat Ma’suma (salamu za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), na pia kwa familia yake tukufu pamoja na watoto wake wasomi na waheshimiwa wa mwanazuoni huyo mchamungu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amnyanyue daraja mwanazuoni huyo Wakiungu, na awajaalie subira na malipo kwa waliobaki nyuma yake, ndugu na jamaa zake, wapenzi wake na wale waliokuwa wakifuata hukumu zake.

Jumuiya ya Walimu wa Hawzah ya Qom, Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha