Jumatatu 3 Agosti 2026 - 11:45
Chuki dhidi ya Uislamu yazidi kuongezeka nchini Kanada

Hawza/ Waislamu wa jiji la Winnipeg wametangaza kuwa Jumatano iliyopita watu wawili walifyatua risasi kuelekea kuta za msikiti wao kwa kutumia silaha.

Kwa mujibu wa Idara ya Tafsiri ya Shirika la Habari la Hawza, Waislamu waliokusanyika katika Msikiti wa Winnipeg kwa ajili ya Swala ya Ijumaa walielezea masikitiko yao kutokana na matukio yanayotokana na kuenea kwa chuki dhidi ya Uislamu nchini Kanada. Katika mahojiano yao walisema kuwa; msikiti na Swala ya Ijumaa daima vimechangia maendeleo ya kijamii katika jamii yao na vimekuwa vikibeba ujumbe wa amani, umoja na utulivu.

Waliongeza kuwa: "Kwa masikitiko makubwa, usiku wa Jumatano watu wawili walifyatua risasi kutoka nje kuelekea kuta za msikiti." Polisi, baada ya kufanya uchunguzi, walitangaza katika taarifa yao kuwa mbali na msikiti, kuta na madirisha ya nyumba zilizoko jirani pia ziliharibiwa kutokana na mashambulizi hayo ya risasi.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, uchunguzi kuhusu wahusika wa tukio hilo bado unaendelea, tukio hilo lilitokea majira ya saa nne usiku, na kamera za ulinzi (CCTV) zilinasa matukio yote.

Bw. Yasser Al-Mustafa, mmoja wa Waislamu wanaoishi katika eneo hilo, alisema katika mahojiano: "Hili ni tukio la kushtua, mimi hushiriki Swala ya Ijumaa katika msikiti huu kila wiki, matukio kama haya hayatufanyi tubaki majumbani kwa hofu; badala yake, yameongeza umoja wetu, na hatutaruhusu hofu yoyote ipenye kupitia mianya yoyote iliyopo."

Chanzo: CBC News.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha