Jumatatu 3 Agosti 2026 - 23:34
Kongamano la Wahubiri wa Afrika Lafanyika Karbala; Watoa Mada Wahimiza Umoja, Kuieneza Dini na Kuwatetea Wanaodhulumiwa

Hawza/ Katika mwendelezo wa shughuli za maadhimisho ya Arubaini ya Imam Hussein (as), Jumuiya ya Aimmat Huda't imefanya Kongamano la Wahubiri wa Afrika mjini Karbala, likiwakutanisha wahubiri na wanazuoni kutoka nchi mbalimbali za Afrika kwa lengo la kujadili nafasi ya wahubiri katika kueneza mafundisho ya Uislamu na kuimarisha umoja wa Waislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kongamano hilo lilianza kwa kisomo kitakatifu cha Qur'ani Tukufu kilichoongozwa na Dkt. Sheikh Jawad Amini.

Akifungua kongamano hilo, Dkt. Sheikh Haashim Abu Khamsin alizungumzia nafasi ya ziara ya Imam Hussein (as) katika kuijenga jamii yenye maadili na uongofu. Alinukuu riwaya mbalimbali kuhusu fadhila za kuzuru kaburi la Imam Hussein (as), huku akisisitiza kuwa; shule ya Imam Hussein (as) ndiyo njia ya kuilea jamii yenye misingi ya haki, uadilifu na kujitolea.

Katika hotuba yake alinukuu pia kauli ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khamenei (ra), isemayo:

«كونوا حسينيين وامضوا حسينيين وسيروا طريق الحسين (ع)»

Baada ya ufunguzi huo, Sheikh Hussein Mwaravino kutoka Kenya aliwasilisha nauha ya kuelezea dhulma walizofanyiwa Ahlulbayt (as) iliyopokelewa kwa hisia na washiriki wa kongamano hilo.

Mapenzi ya Ahlulbayt (as) kwa mujibu wa wafuasi wa madhehebu ya Tasawwuf

Miongoni mwa mada zilizowasilishwa ni ile ya Dkt. Sheikh Muhammad Bamba yenye anuani isemayo; "Mapenzi ya Ahlulbayt (as) kwa Masufi."

Katika mada yake alielezea kwa kina makundi mbalimbali ya Masufi na namna kila kundi linavyoonyesha mapenzi na heshima kwa Ahlulbayt (as). Alibainisha kuwa Masufi huwapa hadhi kubwa Masharifu (Masayyid), ambao katika maeneo mengi ya Afrika wanatambulika kwa jina la Masharifu.

Alisema kuwa; katika baadhi ya jamii za Afrika, Sharifu anapoingia mahali watu husimama kwa heshima, jambo linaloonesha nafasi yao katika jamii, aidha alieleza kuwa katika tawassuli zao, Masufi hutumia ibara maalumu zinazodhihirisha utukufu wa Ahlulbayt (as).

Akihitimisha mada yake, Sheikh Bamba alisema; elimu ya Irfani inahitaji usafi wa moyo na nafsi, na kwamba usafi huo unaonekana wazi katika maisha ya Masufi kutokana na ukaribu wao na Ahlulbayt (as).

Kongamano la Wahubiri wa Afrika Lafanyika Karbala; Watoa Mada Wahimiza Umoja, Kuieneza Dini na Kuwatetea Wanaodhulumiwa

Vikwazo dhidi ya Umoja kati ya Sunni na Shia

Kwa upande wake, Hujatul-Islam, Sheikh Saalim Neganega kutoka Kenya aliwasilisha mada yenye anuani isemayo "Vikwazo Vinavyozuia Mafungamano kati ya Sunni na Shia."

Alitaja changamoto kuu tatu zinazokwamisha umoja huo ambazo ni:

- Vizuizi vya kiitikadi.
- Vizuizi vya kifiqhi.
- Fitna na propaganda zinazoenezwa na maadui wa Uislamu ili kuwagawa Waislamu, ikiwemo kuwazushia baadhi ya Waislamu kuwa wanawatukana Maswahaba.

Alisisitiza kuwa; njia bora ya kujenga umoja ni kufanya mazungumzo (mijadala) yenye kuheshimu misingi na adabu zake ili kuepusha migongano na mifarakano.

Mbinu za Ahlulbayt (as) katika Kueneza Dini

Naye Sheikh Maysara kutoka Sudan aliwasilisha mada kuhusu "Njia Walizozitumia Ahlulbayt (as) katika Kubainisha Dini."

Alieleza kuwa Ahlulbayt (as) walitumia mbinu mbalimbali katika kueneza mafundisho ya Uislamu, zikiwemo:
- Kufanya mijadala ya kielimu (Munadhara), kama ilivyokuwa kwa Imam Ridha (as).
- Kuanzisha madrasa na vituo vya elimu ya dini, kama alivyofanya Imam Ja'far Sadiq (as).
- Kulea wahubiri na wabebaji wa ujumbe wa Uislamu kama Zurara, Hisham na wengineo.
- Kueneza dini kupitia vitendo vyema na maadili, ambavyo ni msingi wa imani na uchamungu.

Aliwahimiza wahubiri kufuata mwenendo wa Ahlulbayt (as) katika kufikisha ujumbe wa dini.

Kongamano la Wahubiri wa Afrika Lafanyika Karbala; Watoa Mada Wahimiza Umoja, Kuieneza Dini na Kuwatetea Wanaodhulumiwa

Mahdawiyya ni Matumaini ya Watu Wote

Sheikh Abdulkarim kutoka visiwa vya Komoro aliwasilisha mada yake kuhusu "Mahdawiyya katika Dini."

Alianza kwa kusoma aya ya Qur'ani Tukufu: وَكَانَ وَعْدًا مَفْعُولًا Alieleza kuwa; imani ya kumsubiri Mwokozi au Mkombozi si jambo linalopatikana katika Uislamu pekee, bali hata dini na tamaduni mbalimbali duniani kama vile Uzartusht, Uhindu, Ubudha na nyinginezo zina fikra zinazofanana kuhusu kuja kwa mwokozi wa mwisho.

Aliongeza kuwa ndani ya Uislamu zipo riwaya nyingi zinazozungumzia kuja kwa Imam Mahdi (as) kama mkombozi atakayeijaza dunia uadilifu baada ya kujazwa dhuluma.

Kongamano la Wahubiri wa Afrika Lafanyika Karbala; Watoa Mada Wahimiza Umoja, Kuieneza Dini na Kuwatetea Wanaodhulumiwa

Kuwanusuru Wanaodhulumiwa ni Wajibu wa Kiislamu

Mada nyingine iliwasilishwa na Sheikh Muhammad Bah kutoka Guine, iliyokuwa na anuani isemayo: "Kuwanusuru Wenye Kudhulumiwa."

Alianza kwa kusoma aya tukufu isemayo:

﴿هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ...﴾

Alifafanua kuwa; miongoni mwa malengo makubwa ya Mitume ni kusimamisha haki na kuwatetea waliodhulumiwa, Akirejea aya za Qur'ani na riwaya kutoka kwa Maasumina (as) alieleza kuwa; Uislamu unawataka waumini kusimama upande wa wenye kudhulumiwa.

Aidha alisema kuwa viongozi wakubwa wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini (ra) na Imam Khamenei (ra), wameonesha kwa vitendo umuhimu wa kuwatetea wanaodhulumiwa duniani. Alibainisha kuwa Imam Khomeini ndiye aliyeasisi Siku ya Kimataifa ya Quds ili kuonesha mshikamano na watu wanaodhulumiwa, hususan wananchi wa Palestina.

Mwisho wa kongamano hilo ulipambwa na hafla ya utoaji wa zawadi kwa watoto walioshiriki mashindano ya maarifa kuhusu Ahlulbayt (as). Washindi kuanzia nafasi ya kwanza walitunukiwa zawadi maalumu, huku watoto wote walioshiriki mashindano hayo wakipewa zawadi za kuwapongeza na kuwahamasisha kuendelea kujifunza mafundisho ya Ahlulbayt (as).

Kongamano hilo limekuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu, kuimarisha mshikamano wa wahubiri wa Afrika na kuhuisha dhamira ya kueneza ujumbe wa Uislamu unaojengwa juu ya elimu, maadili, umoja na utetezi kwa wenye kudhulumiwa.

Kongamano la Wahubiri wa Afrika Lafanyika Karbala; Watoa Mada Wahimiza Umoja, Kuieneza Dini na Kuwatetea Wanaodhulumiwa

Kongamano la Wahubiri wa Afrika Lafanyika Karbala; Watoa Mada Wahimiza Umoja, Kuieneza Dini na Kuwatetea Wanaodhulumiwa

Kongamano la Wahubiri wa Afrika Lafanyika Karbala; Watoa Mada Wahimiza Umoja, Kuieneza Dini na Kuwatetea Wanaodhulumiwa

Kongamano la Wahubiri wa Afrika Lafanyika Karbala; Watoa Mada Wahimiza Umoja, Kuieneza Dini na Kuwatetea Wanaodhulumiwa

Kongamano la Wahubiri wa Afrika Lafanyika Karbala; Watoa Mada Wahimiza Umoja, Kuieneza Dini na Kuwatetea Wanaodhulumiwa

Kongamano la Wahubiri wa Afrika Lafanyika Karbala; Watoa Mada Wahimiza Umoja, Kuieneza Dini na Kuwatetea Wanaodhulumiwa

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha