Jumatatu 3 Agosti 2026 - 10:45
Ushirikiano wa siri kati ya NATO na utawala wa Kizayuni katika vita vya habari na operesheni za kisaikolojia wafichuliwa

Hawza/ Elizabeth Lane, mtafiti na mwandishi wa habari huru, huku akitegemea nyaraka zilizovuja na tafiti zake za uwanjani, amefichua kuwepo kwa mtandao ulioratibiwa kati ya NATO, utawala wa Kizayuni na baadhi ya taasisi za kijasusi za Magharibi kwa ajili ya kuendesha operesheni za vyombo vya habari, udhibiti wa taarifa katika majukwaa ya kidijitali na kampeni za kuwaharibia sifa waandishi wa habari huru.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kikinukuu Islami Analysis, Elizabeth Lane, mtafiti na mwandishi wa habari huru, katika mahojiano na Tucker Carlson, alifichua kile alichokiita ushirikiano wa siri kati ya NATO na utawala wa Kizayuni katika uwanja wa vita vya habari na operesheni za kisaikolojia.

Akitumia nyaraka zilizovuja na matokeo ya uchunguzi wake wa uwanjani alisema kuwa; akaunti za propaganda zinazohusishwa na utawala wa Kizayuni pamoja na mitandao ya roboti za mtandaoni (bots) zinazoiunga mkono NATO nchini Ukraine zinafanya kazi kwa uratibu ili kuelekeza maoni ya umma na kuwashambulia waandishi wa habari huru.

Ushirikiano wa mitandao ya propaganda ya Israel na roboti za Ukraine

Lane alisema kuwa; alipokuwa akichunguza shughuli za propaganda katika mitandao ya kijamii aligundua uhusiano kati ya akaunti za propaganda zinazounga mkono utawala wa Kizayuni na roboti za mtandaoni zinazoiunga mkono Ukraine na NATO.

Aliongeza: "Propaganda hutengenezwa kwanza na wanahabari wanaoiunga mkono Israel, kisha mtandao wa roboti za Ukraine unaohusishwa na NATO huiunga mkono na kuisambaza kwa nguvu zaidi."

Pia alisema kuwa; wakati wa kampeni zilizoratibiwa dhidi yake, alipokea ujumbe uliokuwa na maneno: "Kwa heshima, kutoka kwa Zelenskyy," uliotumwa na akaunti hizo.

Mradi wa NATO mwaka 2019

Mtafiti huyo aliongeza kuwa; mwaka 2019, NATO kupitia Kituo cha Mawasiliano ya Kimkakati (STRATCOM) ilitekeleza mradi wa kupima uwezo wa kudhibiti na kuelekeza mitandao ya kijamii bila kutoaa tahadhari.

Kwa mujibu wake, mradi huo ulifanyika kwa ushirikiano na kampuni iitwayo Singularix katika mji wa Kharkiv nchini Ukraine, ambapo mamia ya maelfu ya akaunti za watumiaji zilitumika kwa maoni na mijadala ya kughushi kwa lengo la kuathiri maoni ya umma.

Mradi wa "Integrity Initiative"

Lane pia alizungumzia mradi unaoitwa Integrity Initiative, akidai kuwa mpango huo, uliokuwa ukifadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza na kutekelezwa kupitia taasisi ya Institute of Statecraft, ulikuwa na lengo la kupambana na kile kilichoitwa "taarifa potofu za Urusi", lakini kwa vitendo ulitumika kuwaondoa katika uwanja wa umma na kuwavunjia heshima wanasiasa na waandishi wa habari huru.

Alisema kuwa Jeremy Corbyn, aliyekuwa kiongozi wa Chama cha Labour nchini Uingereza, pamoja na Pedro Baños, mwanajeshi wa Hispania, ni miongoni mwa watu waliolengwa na mradi huo kupitia kampeni za tuhuma katika vyombo vya habari.

Nafasi ya baadhi ya wanahabari

Lane pia alisema kuwa watu kama Ben Nimmo, Jessica Aro na Peter Pomerantsev walikuwa na nafasi muhimu katika mtandao huo, na walitumia hadhi yao ya vyombo vya habari kuwashutumu wakosoaji kwa kuwahusisha na Urusi.

Pendekezo la malipo kwa wanajeshi wa zamani wa Marekani

Katika sehemu nyingine ya mahojiano hayo, Lane alisema kuwa; mfuko wa Ukraine unaojulikana kama United24 uliwapa baadhi ya wanajeshi wa zamani wa vikosi maalumu vya jeshi la Marekani pendekezo la kulipwa dola za Marekani 10,000 kwa kila video watakayozalisha kwenye YouTube kuunga mkono Ukraine na NATO, pamoja na mapato ya matangazo yanayoweza kufikia dola 40,000.

Lane aliongeza kuwa, kwa mujibu wa wanajeshi hao, baada ya kukataa pendekezo hilo, baadhi yao walituhumiwa kushirikiana na Urusi, taarifa zao zikapelekwa katika maeneo yao ya kazi na wakawekwa chini ya shinikizo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha