Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mkuu wa ofisi ya mwendesha mashtaka ya Umma nchini Bahrain amesema kuwa ofisi hiyo imeanza mchakato wa kukata rufaa katika Mahakama ya Juu ya Rufaa (Tamyiz) dhidi ya hukumu iliyomtangaza Sheikh Ahmad Isa Al-Haiki, mwanazuoni wa Kishia aliyekuwa amekamatwa kuwa hana hatia. Aidha, mashtaka mapya pia yamebuniwa dhidi yake.
Ofisi ya mwendesha mashtaka ya umma imeongeza kuwa; uchunguzi unaendelea kuhusu shughuli zake zinazohusiana na ukusanyaji wa mali ya «faradhi ya Khums», jambo linalodaiwa kufanywa kinyume na masharti ya sheria. Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Bahrain (BNA), Ofisi ya mwendesha mashtaka ya umma inaendelea kuwasilisha kesi hiyo mahakamani.
Hapo awali, mahakama moja ya Bahrain, baada ya awali kutoa hukumu ya kifungo cha maisha katika kesi hiyo hiyo, baadaye ilitoa hukumu ya kumtakasa Sheikh Al-Haiki na kumwona hana hatia. Hukumu hizi zinatolewa katika utekelezaji wa ajenda ya mamlaka za Bahrain ya kutunga mashtaka dhidi ya raia wa Kishia. Hatua hizi ni sehemu ya kampeni ya kulipiza kisasi inayowalenga mamia ya raia, baada ya vyombo vya kijeshi vya Bahrain kushindwa kukabiliana na Iran kufuatia mashambulizi ya makombora ya Iran dhidi ya kambi na maslahi ya Marekani mjini Manama, wakati wa vita vya uchokozi vilivyoanzishwa dhidi ya Iran na Marekani pamoja na utawala wa Kizayuni, kwa uungaji mkono wa baadhi ya nchi za Ghuba ya Uajemi.
Maoni yako