Ijumaa 12 Desemba 2025 - 20:00
Vijana na Mabinti Wawe ni Wenye Shukrani Kutokana na Jitihada Walizo Zifanya Wazazi Wao Kwao

Hawza/ Hadhrat Ayatollah Jawadi Amoli aliwashauri wasichana na wavulana kuwa wenye shukrani kwa juhudi zilizofanywa na baba na mama kuwaelekea wao.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatollah Jawadi Amoli akizungumzia ulazima na thamani ya kuwaheshimu wazazi wawili alibainisha: Kati ya baba na mama, ingawa tabu anayoipata baba katika kutafuta makazi, matumizi na mavazi si ndogo au ni kubwa, lakini tabu ya kubeba ujauzito, kulea mtoto mchanga na kunyonyesha ni taabu inayochosha sana. Hili linakumbushwa ili vijana wawe ni wenye shukrani na mabinti pia wajue kwamba njia hiyo hiyo wanapaswa kukabiliana nayo.

Katika Surah Tukufu Luqman, pale inapozungumziwa kuhusu ushauri juu ya baba na mama, tabu anayoipata mama imetajwa katika aya ya kumi na nne ya Surah Tukufu Luqman ni hii:


«وَوَصَّیْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَیْهِ»

Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili.

Kisha tabu ya mama ikaelezewa pia kwa kusema:


«حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْناً عَلَی وَهْنٍ وَ فِصَالُهُ فِی عَامَیْنِ أَنِ اشْکُرْ لِی وَ لِوَالِدَیْکَ»

Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako

Inatakikana wavulana waithamini nafasi ya mama na wasichana wajifunze desturi ya kuwa mama kutokana na muktadha huu.

Darsa ya Tafsiri 95/1/30 sawa na 18 Aprili 2016

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha