Jumanne 27 Januari 2026 - 16:00
Ghasia za hivi karibuni zilikuwa mapinduzi ya kijeshi dhidi ya dini na watu / Viongozi wa ghasia wanahesabiwa kifiqhi kuwa ni “maharibu”

Hawza/ Mjumbe wa mafaqihi wa Baraza la viongozi alisisitiza: Imam Khomeini (rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) katika kitabu chake cha "Tahrir al-Wasilah" anaeleza wazi kwamba mtu yeyote anayechukua hatua za kueneza hofu, ukosefu wa usalama na ufisadi katika ardhi ni muharib, na hukumu yake iko wazi. Bila shaka yoyote, viongozi wa kihalifu wa ghasia hizi wanahusika na cheo hiki cha kifiqhi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami, katika mkutano mkubwa wa wanazuoni wa Qom uliolenga kulaani matusi ya magaidi wa Kimarekani na Kizayuni kwenye ghasia za hivi karibuni dhidi ya Qur’ani Tukufu na vitakatifu vya Kiislamu, pamoja na kuonesha uungaji mkono thabiti kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo katika Madrasa ya Elimu ya Kidini ya Fayziyyah mjini Qom, akirejelea historia ya mikusanyiko ya kimapinduzi na yenye hamasa ya wanazuoni katika kipindi cha miaka 47 iliyopita, alisema: Mkutano huu ni mwendelezo wa mikutano ile ya kiheshima na ya hamasa ambayo katika vipindi tofauti imeandaliwa na Jumuiya ya Walimu Wakuu, Baraza Kuu la Hawza na Uongozi wa Hawza.

Kupambana na dini; lengo la kwanza la wachochezi wa ghasia

Akirejelea harakati za hivi karibuni nchini Iran, aliongeza kusema: Harakati hizi zilibuniwa na Marekani na utawala wa Kizayuni, na lengo lao la kwanza lilikuwa ni dini. Qur’ani Tukufu inaonya wazi kwamba maadui daima wanataka kuwarejesha Waumini kutoka kwenye dini yao, na yaliyotokea katika siku hizi ni mfano wazi wa mapambano haya.

Mjumbe wa mafaqihi wa Baraza la uongozi aliongeza kusema: Kuchomwa Qur’ani kwa mpango maalumu, kuchomwa moto mamia ya misikiti, kuharibiwa Husseiniyya, kushambuliwa makaburi matukufu, kuchomwa kwa miongo kadhaa ya misala na ofisi za Maimamu wa Swala za Ijumaa, na kuuawa kishahidi wanazuoni saba vijana, yote yanaonesha kuwa suala kuu lilikuwa ni kupambana na dini.

Imamu wa muda wa Swala ya Ijumaa ya Tehran, akikanusha madai ya maadui kuhusu hali ya kidini ya taifa la Iran, alisema: Baadhi ya maadui walidai kwamba Wairani wamejitenga na dini, lakini jibu liko wazi; hawa waliokuwa vibaraka ndio waliounguza Qur’ani, si taifa lenye imani la Iran. Watu hawa, mbele ya wimbi kubwa la wananchi, hawana uzito wowote.

Ayatullah Khatami aliendelea kusema: Hata makanisa pia yalichomwa moto katika matukio haya, jambo linaloonesha kuwa mkondo huu una chuki ya kina dhidi ya asili ya dini yenyewe. Qur’ani Tukufu inabainisha kwamba kama kusingekuwa na ulinzi wa watu dhidi ya watu, vituo vyote vya kidini vingeharibiwa, na uzoefu wa siku hizi ni ushahidi wazi wa ukweli huu wa Qur’ani. Mjumbe wa mafaqihi wa Baraza la viongozi, huku akisisitiza umuhimu wa kuwepo katika uwanja, alisema: Tusipokuwepo, maadui wa dini wataharibu kila alama ya dini. Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, taifa la Iran na Hawza za elimu ya kidini daima zipo katika uwanja wa kuitetea dini.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, huku akirejelea uhalifu uliofanywa katika matukio haya, alisema: Kuua watoto wadogo na watu wasio na hatia kulifichua uso halisi wa watendaji wa fitna hii, na kuonesha kwamba yaliyotokea yalikuwa ni mapinduzi ya kijeshi dhidi ya watu na maadili ya kidini.

Matukio ya hivi karibuni yalikuwa “mapinduzi kamili dhidi ya watu”

Ayatullah Khatami, huku akisisitiza kwamba matukio ya hivi karibuni yalikuwa “mapinduzi kamili dhidi ya watu”, alisema: Katika matukio haya, watoto wasio na hatia wa miaka miwili, mitatu na minane waliuawa kishahidi, na kwa jumla watu 2,427 walipoteza maisha yao. Uhalifu huu unaonesha kwamba hatukuwa tunakabiliwa na harakati ya kawaida au maandamano, bali ni mradi mkali na uliopangwa.

Akielezea uharibifu uliofanywa, aliongeza kusema: Magaidi hawa wa mapinduzi ya kijeshi waliharibu zaidi ya vifaa 600 vya umma, wakaharibu magari binafsi 800 ya wananchi, wakachoma mamia ya mabasi, na wakachoma shule 200, mahali pa elimu ya watoto wa taifa hili. Aidha, vituo vya Basij, nyumba binafsi 300, maduka takriban 700 na vituo 24 vya mafuta vilishambuliwa na kuharibiwa.

Mjumbe wa Jumuiya ya Walimu Wakuu wa Hawza ya Qom alisisitiza: Vitendo hivi ni mfano wazi wa uharibifu katika ardhi. Qur’ani Tukufu katika aya ya 33 ya Suratul Ma’idah inasema:

“Hakika malipo ya wale wanaompingana na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wanaofanya ufisadi katika ardhi si chochote ila wauawe, au wasulubiwe, au wakatwe mikono yao na miguu yao kwa upande tofauti, au wafukuzwe kutoka katika nchi; hiyo ni fedheha kwao duniani, na Akhera watapata adhabu kubwa.”

Ayatullah Khatami aliendelea: Harakati hizi zilikuwa mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa dhidi ya mfumo wa Kiislamu; mapinduzi yaliyoporomoka ndani ya chini ya saa 48. Wabunifu wa fitna hii waliingia uwanjani kwa ndoto ya kurudia mapinduzi ya 28 Mordad, lakini ndoto hizi, kama za mababu zao, zilifukiwa kaburini.

Akirejelea hasara kwa vikosi vya usalama na polisi, alisema: Magari na vifaa 2,221 vya Faraja na Basij viliharibiwa, vituo 49 vya polisi vilishambuliwa, na majengo 404 ya serikali yalivamiwa. Takwimu hizi zinaonesha kuwa lengo lilikuwa ni kupambana moja kwa moja na mfumo wa Kiislamu.

Mjumbe wa mafaqihi wa Baraza la viongozi, akiwashukuru wanazuoni na wananchi, alisema: Kwa uwazi na kwa fahari nasema kwamba nyinyi wanazuoni, bega kwa bega na wananchi, mlizima mapinduzi haya hatari. Wengi wa waliouawa kishahidi katika matukio haya walikuwa wapita njia na watu wasio na hatia kabisa, wasiokuwa na uhusiano wowote na wachochezi wa ghasia, na kuwapa hukumu ya shahidi ni jambo sahihi kabisa.

Vyeo vinne vya kifiqhi vya uhalifu kwa viongozi wa ghasia

Ayatullah Khatami, akirejelea kufichuliwa kwa asili ya ghasia, alisema: Vyombo vya habari vya taifa katika siku za hivi karibuni vimefanya kazi nzuri katika kufichua uhalifu wa viongozi wa ghasia. Viongozi hawa wana vyeo vinne vya kifiqhi vya uhalifu ambavyo, kwa mujibu wa fiqhi ya Kiislamu, vinastahili adhabu kali zaidi.

Akavifafanua vyeo hivyo vinne kama ifuatavyo:

Cheo cha kwanza: Muharib (mwenye kuupiga vita uislamu).
Imam Khomeini (rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) katika "Tahrir al-Wasilah" anasema wazi kwamba mtu yeyote anayechukua hatua za kueneza hofu, ukosefu wa usalama na ufisadi katika ardhi ni muharib, na hukumu yake iko wazi. Bila shaka viongozi wa kihalifu wa ghasia hizi wanahusika na cheo hiki.

Cheo cha pili: Baghiy (uasi).
Sheikh Tusi katika kitabu "Al-Khilaf" anasema wazi kwamba yeyote atakayesimama dhidi ya Imam mwadilifu, hukumu ya uasi inamhusu. Muhaqqiq Hilli pia katika "Shara’i al-Islam" anasisitiza kwamba kupigana na anayemuasi Imam mwadilifu ni wajibu, iwe uasi huo ni wa wazi au wa siri.
Mwandishi wa "Jawahir al-Kalam", juzuu ya 21, anasema wazi kuwa hakuna tofauti ya maoni miongoni mwa Waislamu, bali hata Waumini, kuhusu hukumu hii, na suala hili limekubaliwa kwa makubaliano kamili ya Umma wa Kiislamu.

Cheo cha tatu: Mufsidi katika ardhi (مفسد فی‌الارض).
Kiwango cha uhalifu, uharibifu, mauaji ya wasio na hatia, kueneza hofu katika jamii, na kushambulia mali za umma na binafsi, kwa wazi ni mfano wa ufisadi katika ardhi.

Cheo cha nne: Muuaji.
Kuuawa kishahidi kwa watoto, wananchi wa kawaida na wapita njia wasio na hatia kunawafanya watu hawa wahesabiwe kuwa wauaji wa kukusudia, na kifiqhi hakuna shaka yoyote juu ya hili.

Ulazima wa utekelezaji thabiti wa hukumu

Mjumbe wa Jumuiya ya Walimu Wakuu wa Hawza ya Qom huku akisisitiza ulazima wa utekelezaji thabiti wa hukumu, alisema: Kwa kuzingatia vyeo hivi vya kifiqhi, adhabu kali zaidi kwa viongozi wa ghasia ni hukumu iliyo wazi ndani ya fiqhi ya Kiislamu.

Kwa bahati nzuri, Mkuu wa Mahakama Kuu amesisitiza mara kadhaa kwamba atashughulikia kesi hizi kwa uthabiti, na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa nchi pia amesisitiza msimamo huu. Wananchi wanasubiri kuona uthabiti huu kwa vitendo.

Ayatullah Khatami aliwagawanya wachochezi wa ghasia katika makundi matatu:

1. Kundi la kwanza: Viongozi na wabunifu wakuu — hukumu yao iko wazi.
2. Kundi la pili: Watekelezaji wa uwanjani walio na ufahamu na wanaoshirikiana na mkondo wa kuipindua serikali.
3. Kundi la tatu: Waliodanganywa, ambao hawakuwa na nia ya kupindua mfumo wala hawakushiriki katika uhalifu.

Kukosoa upotoshaji wa aya za Qur’ani kwa ajili ya kuunga mkono ghasia

Akikosoa upotoshaji wa aya za Qur’ani katika kuunga mkono wachochezi wa ghasia, alisema: Baadhi walitumia vibaya aya ka vile aya isemayo “Kwa rehema ya Mwenyezi Mungu ulikuwa mpole kwao” ili kuwalinganisha waliodanganywa na wahalifu, ilhali aya hiyo inawahusu wale wasiokuwa washirika wa uadui na uhalifu, si wale waliolowesha mikono yao damu za watu.

Alisisitiza: Kuhusu waliodanganywa, inapaswa kutekelezwa njia ile ile aliyofuata Amir al-Mu’minin (a.s.) kama ilivyo katika Nahjul Balagha — njia ya uongofu, marekebisho, malezi na kuwarudisha katika njia ya haki, si kuwapendelea wahalifu.

Ayatullah Khatami aliongeza: Inatarajiwa kutoka kwa Mahakama hata kwa waliodanganywa kutekeleza adhabu za kuzuia ili jamii isishuhudie tena ghasia kama hizi.

Malengo ya adui katika vita mseto vya hivi karibuni

Akirejelea malengo ya adui katika vita hivi, alisema: Moja ya malengo makuu ya adui katika vita hivi na katika mapinduzi haya ya kigaidi ilikuwa ni nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi. Hivi karibuni Rais wa Marekani kwa lugha ya kidikteta alisema kuwa taifa la Iran linapaswa kufikiria uongozi mwingine; kauli hii, kabla ya kuwa matusi kwa taifa la Iran, ni fedheha kwa taifa la Marekani.

Alisisitiza kuwa: Uongozi katika Jamhuri ya Kiislamu si uongozi wa kisiasa tu, bali una mizizi ya kina katika mfumo wa itikadi ya Kishia, ukiwa ni mwendelezo wa wilaya ya kidini na uwakilishi wa jumla wa Imam wa Zama (a.j.).

Akabainisha kwamba: Ulinzi wa taifa la Iran kwa wilaya si kauli ya kisiasa, bali unatokana na imani, itikadi na uhusiano wa kina wa moyoni na njia ya Ahlul Bayt (a.s.).

Kukosoa baadhi ya tamko na misimamo ya ndani

Ayatullah Khatami alikosoa baadhi ya matamko ya ndani akisema: Hivi karibuni yametolewa matamko ambayo kwa sura yanaonekana kama ushauri, lakini kwa maudhui ni marudio ya maneno ya Trump na Netanyahu. Hii ni fedheha na si sauti ya taifa la Iran.

Mwisho, Ayatullah Khatami aliwashukuru waliohudhuria mkusanyiko wa wanazuoni wa Qom na kusema: Nawashukuru kwa dhati nyinyi watu wa dini wenye hamasa. Wale walioteketeza misikiti, Qur’ani na makazi kwa makusudi walifanya uhalifu ambao hata Wamongolia hawakuwahi kuufanya. Lakini kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, wachochezi wa fitna walifedheheka.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha