Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami, mjumbe wa Mafaqihi wa Baraza la Kulinda Katiba, ametoa ujumbe ambao ndani yake ameyaelezea mazishi ya Imam Shahidi kuwa ni "tukio lisilo na mfano katika karne" na "udhihirisho wa mshikamano kati ya dini na taifa," kisha akachambua jumbe za kimkakati za tukio hilo la kihistoria.
Mjumbe huyo wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom, katika ufafanuzi wake, amesisitiza umuhimu wa kutambua na kulinda umoja katika misingi ya pamoja na kuimarisha uhusiano kati ya kujitenga na maadui na kutoa bai'a kwa mrithi wa Wilayah.
Matini ya ujumbe wa kimkakati wa Ayatullah Khatami ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
«وَلَا تَهِنُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَنْتُمُ الْأَعْلَوْنَ إِنْ کُنْتُمْ مُؤْمِنِینَ»
Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini.
(Surat Aal Imran: 139)
Yaliyoshuhudiwa katika siku hizi kwenye mazishi ya Imam Shahidi na familia yake, yaliyofanywa na wananchi wa Iran na Iraq, kwa hakika ni "tukio lisilo na mfano la karne," na yameonesha daima uhusiano wa kina kati ya mataifa haya mawili. Maneno yaliyotumiwa na vyombo vya habari kama vile "mazishi makubwa zaidi ya karne," "uumbaji wa hamasa isiyo na kifani," "gwaride la ushindi," "mahudhurio ya watu milioni ishirini," "kubadilika kwa mizania," na "sauti ya wazi ya mitaani dhidi ya propaganda za maadui," yote yanaonesha kutokea kwa tukio kubwa na la kushangaza ndani ya Iran.
Pamoja na kutoa shukrani na pongezi kwa washiriki wote wa mazishi hayo, jambo la msingi ni kuzitambua jumbe zinazoakisiwa na tukio hili lisilo na mfano na kuzilinda; kwa sababu ni lazima jumbe hizi zitambuliwe na zihifadhiwe.
Yaliyotokea katika siku hizi katika nchi yetu pendwa yalikuwa ni mazoezi makubwa; mazoezi ya kushikamana na dini, utii kwa Wilayah na kuipenda nchi. Hapana shaka kwamba adui, kupitia upotoshaji, uzushi na kuchochea migawanyiko, anataka kubadilisha mazingira haya yenye kustahili kupongezwa. Hivyo ni lazima adui ashindwe pia katika medani hii, na jumbe za mazingira haya matakatifu zilindwe.
Baadhi ya jumbe hizo ni hizi:
1. Ujumbe wa kuamini dini na kuzipenda thamani za dini:
Wananchi, kwa vitendo na kwa kauli zao, wametangaza kwamba wamesimama chini ya bendera ya dini na wataendelea kusimama imara.
2. Ujumbe wa mshikamano kati ya Marjaiyyah na Mfumo wa Kiislamu:
Mar'ajii wakuu, iwe kwa kutoa ujumbe au kwa kuswalisha Swala ya Maiti juu ya mwili wa Imam Shahidi na familia yake, walisisitiza uhusiano huu.
3. Ujumbe wa kuunganika kwa mapenzi ya dini na nchi ya Kiislamu:
Wananchi walimheshimu kwa moyo wote kiongozi ambaye alikusanya kwa kiwango cha juu kabisa hazina hizi mbili, na wakamtaja kuwa "mzalendo mkubwa zaidi."
4. Ujumbe wa kujitenga na kulipiza kisasi dhidi ya maadui wenye chuki wa Mapinduzi:
Sherehe hii iliwachukiza zaidi maadui. Bendera nyekundu za kisasi zilikuwa ushahidi kwamba madai haya si tu yanatokana na mantiki ya Qur'ani na Fiqhi, bali pia ni haki isiyopingika inayotambuliwa katika sheria za kimataifa.
5. Ujumbe wa kutoa bai'a kwa mrithi wa Wilayah, Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, mwema baada ya mwema:
Kiongozi mkubwa ambaye ameendeleza kwa uthabiti njia ya Maimamu wawili wa Mapinduzi na ameendelea kuipeperusha bendera hii takatifu.
6. Umoja katika misingi; urithi wa Maimamu wawili wa Mapinduzi:
Umoja na mshikamano hupata maana yake ndani ya misingi. Tofauti za mitazamo, maadamu hazisababishi mgawanyiko, si jambo lenye madhara, lakini kile tulichokishuhudia katika siku hizi ni "umoja katika misingi," ambao Imam Khomeini (ra) na Imam Shahidi waliusisitiza daima, na ambao ni lazima ulindwe kwa nguvu zote.
7. Udhihirisho wa wasia wa Qur'ani na Ahlul-Bayt (as) katika hafla za kumuenzi Imam Shahidi:
Ujumbe wa kusimama kidete na kutokuchoka kwa wananchi, katika mikusanyiko mikubwa ya miezi ya karibuni na pia katika hafla za kumuenzi Imam Shahidi, umethibitisha kwamba huu ndio wasia wa Qur'ani na Ahlul-Bayt (as). Bila shaka, umma ambao umeufanya uchovu uchoke, na umesimama imara kama mti wa mvinje, ndio utakaoshinda katika medani.
Mwishoni, kwa fahari kubwa kabisa, ninajiona kuwa mtumishi na mwenye kubusu mikono ya umma huu ambao umeutukuza Uislamu na madhehebu ya Ahlul-Bayt (as).
Wassalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh
Sayyid Ahmad Khatami
Maoni yako