Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini kamili ya ujumbe wa Ayatullah al-Udhma Muzahirii, mmoja wa Mara'jii Wakuu wa Taqlid, kwa mnasaba wa hafla tukufu za kuuaga na kuuzika mwili mtukufu wa Kiongozi na Qaid Shahidi wa Umma wa Kiislamu, ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
«یَا أَیَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ، ارْجِعِی إِلَی رَبِّکِ رَاضِیَةً مَرْضِیَّةً، فَادْخُلِی فِی عِبَادِی، وَادْخُلِی جَنَّتِی»
Hafla tukufu ya mazishi ya mwili mtakatifu wa Kiongozi Mujahid na Qaid Shahidi wa Umma wa Kiislamu, Ayatullah Shahidi Sayyid Ali Khamenei (ra), iliyofanyika kwa ushiriki wa mamilioni ya wananchi wenye uelewa na heshima wa Iran pamoja na Waislamu mashujaa na watukufu wa Iraq, imeonesha mandhari za kushangaza ambazo kwa mara nyingine zimethibitisha uimara na ustahimilivu wa taifa hili lililohuishwa katika kusimama juu ya malengo makubwa ya Uislamu na Iran. Vilevile imeonesha kwa wazi kina cha mapenzi na upendo wao kwa Kiongozi huyo Shahidi mtukufu, ikaweka wazi mbele ya dunia utukufu, nguvu na fahari ya Umma wa Kiislamu, na kuwazamisha maadui walioapa kuipinga nchi hii katika dimbwi la kushindwa, kukata tamaa na kutengwa.
Amani, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwashukie wananchi hawa waumini na wenye kusimama imara katika njia ya haki, ambao katika kila kipindi nyeti cha historia wamekuwa wakitekeleza kwa namna bora zaidi jukumu lao la kuadhimisha alama za Mwenyezi Mungu na kulinda malengo ya Kiislamu, huku wakiwasukuma maadui wa Uislamu, Mapinduzi ya Kiislamu na wanaoitakia mabaya nchi ya Imam wa Zama (arwahuna fidah) kuelekea katika hali ya kukata tamaa na kushindwa zaidi.
Kauli za kipuuzi za hivi karibuni za Rais muhalifu na mwenye historia nyeusi wa Marekani za kulitishia taifa kubwa la Iran ni ushahidi wa wazi wa kiwango cha fedheha, kushindwa, hofu na woga wake mbele ya taifa hili kubwa la Iran.
Sasa Kiongozi huyo Shahidi mwenye cheo cha juu, ambaye alikuwa mwalimu na muongozo thabiti wa taifa, baada ya maisha ya kujitolea kwa ikhlasi katika njia ya haki, amepokea malipo ya jihadi, subira na uimara wake kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, na kwa mikono ya waovu wahalifu wa zama hizi amefikia neema kubwa ya shahada. Miili iliyokatwakatwa vipande vya Kiongozi huyo Shahidi pamoja na watu wa nyumba yake tukufu imepumzishwa karibu na Imam Mwenye Huruma, Ali ibn Musa ar-Ridha (as), huku akiikabidhi amana kubwa ya Mapinduzi matukufu ya Kiislamu kwa taifa hili waaminifu. Roho yake imepata mapumziko katika ukaribu wa Mwenyezi Mungu, na jina pamoja na kumbukumbu yake itabaki milele katika historia tukufu ya taifa hili lenye heshima.
Sasa tumebaki na majonzi ya kuondokewa na Imam wetu mtukufu aliyefariki pamoja na Kiongozi wetu Shahidi mwenye cheo cha juu (quddasa sirrahumā) na amana hii yenye thamani kubwa waliotuachia viongozi hawa wawili watukufu. Siri kuu ya kuilinda amanah hii nyeti ni kuwa na baswira, kudumisha umoja wa taifa na kufuata Wilayatul Faqih pamoja na Kiongozi mwenye baswira na uongofu wa Mapinduzi. Jambo hili, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu, limejitokeza wazi katika miezi minne iliyopita kupitia mikusanyiko ya usiku ya wananchi hawa wenye heshima na waliodumu katika njia ya Qur'ani na Ahlul-Bayt (as), na baadaye katika mazishi makubwa ya Kiongozi wetu Shahidi mtukufu. Hali hiyo imewafurahisha marafiki wote wa Uislamu na Iran, na kuwakatisha tamaa maadui pamoja na wageni.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa neema na fadhila hizi za ukarimu. Tunaibusu mikono ya nguvu ya taifa hili la waumini na wapiganaji, na tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, chini ya kivuli cha uangalizi maalumu na dua inayokubaliwa ya Hadhrat Baqiyyatullah al-A'dham, Sahib al-Amr, Imam Mahdi al-Mau'ud (aj), awazidishie wananchi hawa heshima, utukufu, nguvu na kuinuliwa zaidi.
Tunatumaini kwamba Mwenyezi Mungu Mshindi na Mlipa kisasi atazituliza nyoyo zilizoumia za taifa hili waaminifu kwa kulipiza kisasi cha damu takatifu ya Kiongozi Shahidi na mashahidi wote wa uhalifu wa madhalimu wa Marekani na Wazayuni, hususan watoto wasio na hatia wa Minab, makamanda mashujaa, wanazuoni, watumishi wa Uislamu na Waislamu, pamoja na wananchi wengine wasio na msaada na waliodhulumiwa. Pia tunamuomba awaangamize na kuwavunja nguvu maadui waovu na wahalifu wa Uislamu na Iran, awape wote tawfiki zaidi katika kuisaidia dini Yake na kulinda maadili pamoja na malengo ya juu ya Qur'ani Tukufu na Ahlul-Bayt watoharifu (as), na awajaalie viongozi wa mihimili yote mitatu ya dola mafanikio makubwa zaidi katika kulitumikia taifa hili lenye subira na baswira, na katika kupunguza maumivu, mateso na changamoto zinazowakabili wananchi.
«وَلَینْصُرَنَّ اللَّهُ مَنْ ینْصُرُهُ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِی عَزِیزٌ»
Wassalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh.
Maoni yako