Jumatano 1 Julai 2026 - 07:32
Mwinyi Apongeza Msaada wa Iran katika Kuendeleza Uchumi na Maendeleo ya Zanzibar

Hawza/ Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Dkt. Mwinyi amesema hayo jana, tarehe 30 Juni 2026, alipokutana na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania, Mhe. Mohammad Javad Hemmatpanah, aliyefika Ikulu Zanzibar kujitambulisha.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano katika sekta za elimu, teknolojia, viwanda, kilimo, afya, biashara, mafuta na gesi, huku akiikaribisha Iran kuwekeza Zanzibar, hususan katika uchumi wa buluu na viwanda.

Mwinyi Apongeza Msaada wa Iran katika Kuendeleza Uchumi na Maendeleo ya Zanzibar

Kwa upande wake, Balozi Hemmatpanah amepongeza uongozi wa Rais Dkt. Mwinyi kwa mageuzi ya maendeleo Zanzibar na kueleza dhamira ya Serikali ya Iran ya kuendelea kuimarisha ushirikiano na Zanzibar kupitia uwekezaji, kubadilishana uzoefu, maarifa na teknolojia katika sekta mbalimbali.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha