Kwa mujibu wa Kitengo cha Tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sheikh Ahmad Qabalan, Mufti Mkuu wa Jaafaria nchini Lebanon, amesisitiza kwamba; suala kuu ni mamlaka ya kitaifa ya Lebanon, ni mfumo wake wa maridhiano na ushirikiano wa Kiislamu na Kikristo, ambao unapingana na miradi ya Kizayuni ya kuiangamiza nchi hiyo. Alisema kuwa; kupuuza ukweli huu hakumnufaishi yeyote, kwa sababu baadhi ya watu wanacheza nafasi ya watumishi watiifu wa miradi ya Marekani na Uzayuni. Hivyo, yeyote anayesisitiza kubaki katika mazingira yanayoitumikia Tel Aviv, basi aende huko. Aliongeza kuwa; wale wanaolia kwenye Ukuta wa Magharibi (West Wall) tayari wamepoteza dau lao, na leo Muqawama ndio alama ya Lebanon na ndio nembo ya mamlaka yake ya kitaifa. Aidha, kwa kuandaa ushirikiano kati ya jeshi na Muqawama, tutakuwa tumesimama juu ya msingi muhimu zaidi wa kujenga mfumo wa usalama na ulinzi wa taifa.
Sheikh Qabalan aliongeza: Huu ni wakati wa kuilinda Lebanon, kuwaheshimu wapiganiaji wa mamlaka ya taifa la Lebanon na kuhakikisha maamuzi ya kitaifa yanalindwa, si kutekeleza maagizo na masharti ya Marekani. Hasa kwa kuwa Netanyahu, mchinjaji wa Tel Aviv, kutokana na matokeo ya vita hivi sasa amebakia kuwa sehemu ya historia, na hatima yake itakuwa kama ya makaburi ya kisiasa. Wakati huo huo, Lebanon imekuwa nguvu yenye uzito wa kikanda, ambapo athari za uwanja wa kusini zimejiweka zenyewe. Aidha, msimamo wa Iran wa kusisitiza kulindwa kwa mamlaka ya kitaifa ya Lebanon umelifanya leo faili la Lebanon kuwa na nafasi yenye nguvu katikati ya maelewano makubwa kati ya Tehran na Washington.
Aliendelea kusema: Tuna imani kamili na Tehran, na mchezo wa kuitenganisha Lebanon na mazungumzo ya Washington na Tehran kwa manufaa ya mazungumzo ya Kizayuni ya Washington uko wazi kabisa, na hatutatoa nafasi yoyote ya kisiasa wala ya kiusalama kwa jambo hilo. Nguvu inayotaka kuifanya Lebanon kuwa ya Kimarekani haitatawala; wala Lebanon haitakuwa uwanja wa mchezo wa yeyote, hususan Tel Aviv. Mamlaka ya sasa, kwa mtazamo wa kisiasa na wa mamlaka ya kitaifa, inajiangamiza yenyewe, hasa kwa kuwa imelizuia Jeshi la Lebanon kuitetea nchi yake, au angalau kushiriki katika ulinzi wa taifa lake, huku ikiendelea kuudhoofisha mkataba wa kitaifa.
Tutazuia Aina Yoyote ya Uadui Dhidi ya Tehran
Mufti wa Jaafari alisisitiza: Lebanon ni itikadi ya kitaifa na mfumo uliojengwa juu ya maridhiano. Yeyote atakayeupiga mfumo huu wa maridhiano wa Lebanon, atauweka katikati ya janga la kitaifa ambalo halijawahi kushuhudiwa, na bila shaka huo ni uchaguzi hatari sana. Vidole vya Washington, Tel Aviv na makundi yanayochochea mauaji ya kimadhehebu ndivyo vilivyo nyuma ya mchezo huu wa kujiangamiza.
Kwa kuwa tupo katika siku za Imam Hussein (as) na kumbukumbu ya harakati yake kubwa, tunaishukuru Iran ambayo imechangia kwa kiwango kikubwa katika kuilinda mamlaka ya Lebanon, na tunaialika ichukue nafasi ya mshirika na tegemeo la Saudi Arabia nchini Lebanon ili kuzuia moto wa fitna za Marekani na Uzayuni. Lebanon haiwezi kuwa dhidi ya Iran wala dhidi ya Saudi Arabia. Na yeyote atakayetekeleza miradi ya uadui dhidi ya Iran, ataiweka Lebanon kwenye taya za mbwa mwitu wa Marekani. Sisi tutazuia aina yoyote ya uadui dhidi ya Tehran. Wapo wanaofahamu kwamba Marekani ni mshirika wa Israel, dola ya kigaidi katika vita dhidi ya Lebanon, ilhali Iran ni mshirika wa Lebanon katika kutetea mamlaka yake ya kitaifa.
Trump Anatafuta Mbadala wa Netanyahu
Katika muendelezo wa mazungumzo yake alisema: Kwa hiyo, epukeni kucheza na moto, hasa katika masuala ya mamlaka ya kitaifa na mahusiano ya kidini na ya kimaadili. Tuachane na mchezo wa hongo za kisiasa, leo Lebanon, kwa mapenzi na uwezo wa Mwenyezi Mungu, na kwa baraka za kujitolea kwa Muqawama, mateso ya majeruhi wake na subira ya wananchi wake watukufu, inatoka katika vita hatari zaidi ikiwa na ushindi mkubwa zaidi. Haya yanatokea katika Mashariki ya Kati ambayo ndani yake Tehran imekuwa nguvu kubwa ya kikanda, hali hii imepanua nafasi ya maslahi ya mamlaka ya kitaifa ya Lebanon, wakati ambapo Trump anatafuta mbadala wa Netanyahu. Matokeo yake ni kwamba Israel imepoteza uwezo wake wa kuunda sura ya Mashariki ya Kati mpya, na kwa uwepo wa Tehran pamoja na makombora yake mazito, Lebanon imechukua nafasi ya moyo wa mfumo mpya wa Mashariki ya Kati.
Tunataka Kuimarishwa kwa Mamlaka ya Lebanon na Kupatikana kwa Washirika Waaminifu wa Kikanda, Sio Washirika Madhalimu na Wasaliti
Sheikh Qabalan alisema: Tunataka kuimarishwa mamlaka ya Lebanon na kupatikana washirika waaminifu wa kikanda, si washirika madhalimu na wasaliti. Lebanon itasimama imara tu kupitia ushirikiano wa maridhiano na nguvu ya mamlaka yake ya kitaifa. Hakuna jambo lililo muhimu zaidi kwetu kuliko umoja wa Kiislamu kati ya Sunni na Shia, na kamwe hatutauacha. Tunamshukuru kila aliyeilinda Lebanon dhidi ya mchezo na fitna hatari zaidi za Marekani na Uzayuni, na pia tunaupongeza Muqawama, mashahidi, majeruhi na waliolazimika kuyahama makazi yao (watu wa Kusini, Dhahiyah na Bonde la Beqaa). Vilevile tunapongeza juhudi za watu binafsi na viongozi wa kitaifa ambao hawakusalimu amri katika nyakati ngumu zaidi za kihistoria za Lebanon.
Mwenye Kumshikamana na Imam Hussein (as) Hataijua Kamwe Maana ya Kushindwa
Mwishoni alisema kuwa: Tunaukumbusha uongozi wa sasa wa Lebanon kwamba; unapaswa kurejea kwa Rais Nabih Berri, na bila yeye hatutakubali ahadi yoyote. Historia yetu ni Imam Hussein (as); hatuna chochote isipokuwa Imam Hussein (as), wala hatuna mbadala wake. Mwenye kuwa na Imam Hussein (as), hataijua kamwe maana ya kushindwa, hata kama majeshi ya wavamizi yataongezeka kwa idadi kubwa, na hata kama fitna za zama zitaendelea kwa muda mrefu kutokana na ujinga wa wapumbavu na njama za maadui.
Maoni yako