Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatullah Jawadi Amuli, mmoja wa Marajii wakubwa wa Taqlidi, aliwasili katika Msikiti Mtukufu wa Jamkaran na kwenye jukwaa la hafla kwa ajili ya kuongoza Swala ya maiti juu ya mwili mtakatifu na mtukufu wa Imam Shahidi pamoja na mashahidi wapendwa wa familia yake.
Marjii huyo wa Taqlidi, alipofika karibu na mwili mtukufu wa Shahidi mpendwa, Hadhrat Ayatullah al-Udhma Imam Khamenei (Quddisa Sirruhu ash-Sharif), pamoja na mashahidi wa familia yake, alitoa heshima zake kwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi na akabusu kilemba chake.

Maoni yako