Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ali Akbar Pourjamshidian, Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya Hafla za Kuaga na Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi, katika mahojiano na taarifa ya habari ya saa nane mchana kupitia televisheni, alisema: Majira ya alasiri ya leo, baada ya kukamilika kwa hafla za mazishi mjini Tehran, miili mitukufu ya Imam Shahidi na familia yake itaandaliwa kwa ajili ya kupelekwa katika mji mtakatifu wa Qom.
Jamkaran; Mwenyeji wa Kiongozi Shahidi
Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya Hafla za Kuaga na Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi aliendelea kusema: Miili mitukufu ya Kiongozi Shahidi na familia yake itawasili katika Msikiti Mtukufu wa Jamkaran kabla ya Swala ya Alfajiri ya Jumanne, na Swala itaongozwa na mmoja wa Marjaa wakuu wa Taqlid.
Pourjamshidian, huku akitangaza njia ya msafara wa mazishi katika mji wa Qom, alisema: Msafara wa mazishi katika mji wa Qom utaanzia katika Msikiti Mtukufu wa Jamkaran kuelekea Haram Tukufu ya Bibi Fatimah Ma'sumah (as), kupitia Barabara ya Mtume Mtukufu Muhammad (saww).
Kwa mujibu wa maelezo yake, baada ya kukamilika kwa mazishi mjini Qom, miili mitukufu itahamishiwa kesho usiku kwenda Najaf Ashraf. Katika Uwanja wa Ndege wa Najaf kutafanyika hafla rasmi ya mapokezi itakayohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa kiraia na kijeshi wa Iraq, pamoja na viongozi wa makabila na watu mashuhuri wa nchi hiyo.
Kuomba Radhi kwa Washiriki wa Mazishi ya Tehran
Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya Hafla za Kuaga na Mazishi ya Mwili Mtukufu wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi pia alikumbusha kwamba: Kutokana na kupewa kipaumbele usalama na afya ya wananchi, hatukuweza kuanza msafara wa mazishi mjini Tehran tangu mwanzo wa njia na kutoka sehemu ya mashariki kabisa ya mji. Tulilazimika kuuingiza msafara wa miili mitukufu katikati ya Barabara ya Azadi, kwa sababu hiyo, tunawaomba radhi kwa dhati wananchi watukufu wa Tehran na wageni wote waliohudhuria hafla hiyo.
Maoni yako