Jumatatu 29 Juni 2026 - 08:55
Bujumbura Yaungana Kumuenzi Imam Hussein (as); Waumini Wafurika Majlisi ya Ashura Nchini Burundi + Picha

Hawza/ Waumini wa Ahlul-Bayt (as) nchini Burundi wamekusanyika kwa wingi katika mji mkuu wa Bujumbura kushiriki kikao kikubwa cha maombolezo ya Siku ya Ashura 1448 Hijria (2026), kwa lengo la kuhuisha kumbukumbu ya shahada ya Imam Hussein (as) pamoja na mashujaa wa Karbala waliouawa kishahidi wakitetea haki, uadilifu na misingi ya Uislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Majlisi hiyo iliongozwa na Sheikh Jamali Kasole, ambaye aliwasilisha muhadhara ulioangazia nafasi ya mapambano ya Imam Hussein (as) katika kulinda dini ya Kiislamu na kusimama dhidi ya dhulma na uonevu, aidha, aliwahimiza waumini kuendelea kufuata maadili, subira na kujitolea mambo ambayo yalivyodhihirishwa na Imam Hussein (as) katika tukio la Karbala.

Mamia ya waumini wakiwemo wanawake, wanaume na vijana, walihudhuria maadhimisho hayo yaliyofanyika katika mazingira ya huzuni na majonzi makubwa. Washiriki walishiriki katika usomaji wa Qur'ani Tukufu, nauha na nyimbo za maombolezo, pamoja na dua na kumbukumbu za msiba wa Karbala.

Katika hotuba yake, Sheikh Jamali Kasole alieleza kuwa; Ashura si tukio la kihistoria pekee, bali ni shule ya kudumu inayofundisha kusimama upande wa haki, kupinga dhulma na kujitolea kwa ajili ya kulinda misingi ya dini na utu wa mwanadamu.

Bujumbura Yaungana Kumuenzi Imam Hussein (as); Waumini Wafurika Majlisi ya Ashura Nchini Burundi + Picha Bujumbura Yaungana Kumuenzi Imam Hussein (as); Waumini Wafurika Majlisi ya Ashura Nchini Burundi + Picha

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha