Jumatano 17 Juni 2026 - 14:14
Maadhimisho ya Muharram Yaanza kwa Ushiriki Mkubwa Mjini Moshi Tanzania + Picha

Hawza/ Msikiti wa Ahlulbayt (as) uliopo mjini Moshi na unaosimamiwa na Taasisi ya Ummulbanin, umeandaa Majlisi ya Kwanza ya Muharram kwa mwaka wa 1448 Hijria (2026), katika mazingira yaliyogubikwa na huzuni, mapenzi na kumbukumbu za mashujaa wa Karbala.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Majlisi hiyo ilifanyika kwa ushiriki mkubwa wa waumini kutoka maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi, ambapo walikusanyika kwa ajili ya kuhuisha ujumbe wa Imam Hussein (as) na kutafakari mafunzo ya mapambano yake dhidi ya dhulma na uonevu.

Katika hafla hiyo ya kiroho na kielimu, washiriki walipata fursa ya kusikiliza mawaidha na mihadhara mbalimbali iliyolenga kuangazia malengo ya mapinduzi ya Karbala na nafasi yake katika kuhuisha maadili ya Kiislamu katika jamii.

Miongoni mwa wahadhiri waliotoa nasaha katika Majlisi hiyo alikuwa Dkt. Abdurrazak Amiri, ambaye aliwasilisha mhadhara wa kina kuhusu kadhia ya Imam Hussein (as), huku akielezea sababu za harakati zake, misingi ya msimamo wake wa kihistoria, pamoja na athari zake endelevu katika ulimwengu wa Kiislamu na harakati za kusimamia haki na uadilifu.

Maadhimisho ya Muharram yanaendelea katika Msikiti wa Ahlulbayt (as) mjini Moshi kwa ratiba mbalimbali za kidini, huku waumini wakihimizwa kushiriki katika vikao hivyo vya maombolezo na kujifunza kwa kina mafundisho yanayotokana na tukio la Karbala.

Maadhimisho ya Muharram Yaanza kwa Ushiriki Mkubwa Mjini Moshi Tanzania + Picha

Maadhimisho ya Muharram Yaanza kwa Ushiriki Mkubwa Mjini Moshi Tanzania + Picha

Maadhimisho ya Muharram Yaanza kwa Ushiriki Mkubwa Mjini Moshi Tanzania + Picha

Maadhimisho ya Muharram Yaanza kwa Ushiriki Mkubwa Mjini Moshi Tanzania + Picha

Maadhimisho ya Muharram Yaanza kwa Ushiriki Mkubwa Mjini Moshi Tanzania + Picha

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha