Jumanne 11 Agosti 2026 - 01:12
Uwepo wa Hawza katika soko la uzalishaji na usambazaji wa elimu duniani ni mkakati wa msingi

Hawza/ Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, amesisitiza kwamba; kuwakilisha Hawza na mafanikio yake katika soko la elimu duniani, pamoja na kwenye vituo vya vyuo vikuu na jumuiya za wasomi na wataalamu nchini Iran na duniani kote, ni mkakati wa msingi ambao unapaswa kufuatiliwa kwa moyo, kwa dhati na kwa nguvu zote.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika juhudi za kutekeleza mikakati mikuu ya Hawza inayolenga kuzifanya tafiti za kidini za Hawza kuwa za kimataifa, na kwa lengo la kuinua nafasi ya kielimu ya Hawza katika mifumo ya kimataifa ya upangaji wa viwango na hifadhidata za marejeo ya kitaaluma duniani, pamoja na ufuatiliaji uliofanywa na Idara ya Tafiti na Mipango ya Utafiti ya Naibu wa Utafiti na kwa uratibu wa Kituo cha Mawasiliano kati ya Hawza na Mfumo wa Elimu, makubaliano yamesainiwa kati ya Naibu Idara za Utafiti za Hawza na Taasisi ya Uwekaji Kumbukumbu na Ufuatiliaji wa Sayansi na Teknolojia ya Ulimwengu wa Kiislamu (ISC).

Makubaliano haya yanaweka mazingira ya kutumia uwezo wa ufuatiliaji wa maendeleo ya sayansi katika kuorodhesha na kuweka katika hifadhidata kazi bora za kielimu za Hawza, pamoja na kuinua viwango vya kitaaluma vya uzalishaji wa tafiti za Hawza. Hii itakuwa hatua madhubuti kuelekea kuifanya Hawza kuwa rejea ya kielimu katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kusisitiza uwepo wa Hawza katika soko la uzalishaji na usambazaji wa elimu duniani

Ayatullah Arafi, Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, pia aliashiria kutiwa saini ya makubaliano haya kuwa ni hatua inayostahili kupongezwa na kushukuriwa, akisisitiza umuhimu wa uwepo wa Hawza katika soko la uzalishaji na usambazaji wa elimu duniani, alisema:

“Pamoja na mitaji yake yote, hazina zake, uwezo wake na fursa ilizonazo, Hawza bado haipo wala haina ushawishi katika njia na mifumo ya fikra na utamaduni duniani kwa kiwango kinachostahili. Tafiti na mafanikio yake kamili hayaonekani katika majarida na vituo vya kitaaluma kwa kiwango kinachostahili; wala hayawasilishwi kwa lugha zinazotumiwa na watu duniani, wala katika mazingira ya mabadiliko ya kielimu na kiteknolojia na anga ya kidijitali, kimsingi kwa mtazamo huo hatuna uzalishaji unaofaa na wa kiwango kikubwa.”

Kuuwakilisha Hawza na mafanikio yake katika soko la elimu duniani

Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, alisisitiza pia jambo hili la msingi kwamba; kuwakilisha Hawza na mafanikio yake katika soko la elimu duniani, pamoja na katika vituo vya vyuo vikuu na jumuiya za wasomi na wataalamu nchini Iran na duniani kote, ni mkakati wa msingi ambao unapaswa kufuatiliwa kwa moyo, kwa dhati na kwa nguvu zote.

Jukumu muhimu la Ayatullah Arafi kwa Naibu wa Utafiti wa Hawza

Ayatullah Arafi pia alieleza kwamba; uwepo wenye ufanisi wa Hawza katika soko la elimu duniani unahitaji busara, tafakuri na fikra, pamoja na kubuni mipango na kuweka ramani ya utekelezaji. Hivyo, alimuagiza Naibu wa Utafiti wa Hawza kushirikiana na manaibu wengine, hususan Naibu wa Masuala ya Kimataifa, pamoja na taasisi na vitengo vya utekelezaji vya Hawza, kulipa jambo hili umuhimu unaostahili, kuibua mpango mpya na kukamilisha njia ambazo tayari zimepitiwa kwa kushirikiana na walimu, watafiti na vituo vya utekelezaji.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha