Jumanne 16 Juni 2026 - 22:00
Wajibu wa Kujilinda Dhidi ya Adui

Hawza/ Ayatullah Makarim Shirazi amejibu istifta (swali la kisheria) kuhusu “wajibu wa kujilinda dhidi ya adui.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Makarim Shirazi ametoa jawabu la istifta inayohusiana na “wajibu wa kujilinda dhidi ya adui”, ambalo tunaliwasilisha kwa wapenda maarifa kama ifuatavyo:

Wajibu wa Kujilinda Dhidi ya Adui

Swali:
Je, ni wajibu kwa Waislamu wote kujilinda dhidi ya mashambulizi ya maadui yanayolenga nchi za Kiislamu?

Jawabu:
Kujilinda dhidi ya mashambulizi ya maadui yanayolenga nchi za Kiislamu na mipaka yake ni wajibu kwa Waislamu wote. Wajibu huu hauhusiani tu na nchi ambayo mtu anaishi ndani yake, bali Waislamu wote duniani wanapaswa kuwa watetezi wa wenzao mbele ya mashambulizi ya wageni dhidi ya nchi za Kiislamu au dhidi ya maeneo matakatifu ya Waislamu.

Maoni yako

You are replying to: .
captcha