Jumatatu 15 Juni 2026 - 17:00
Muharram 1448 H nchini Bahrain; Msimu wa Kusimama Imara na Kudumu Katika Ustahimilivu Chini ya Vikwazo na Vitisho

Hawza/ Ashura ya mwaka huu nchini Bahrain itakuwa tofauti, macho yote yameelekezwa kuona jinsi Wabahrain watakavyohuisha msimu wa maombolezo ya Husseini ambapo Waislamu wengi na Mashia wa Ahlul-Bayt as wanausubiri kwa hamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, likinukuu “Mir’at al-Bahrain”, Ashura ya mwaka huu nchini Bahrain itakuwa tofauti, macho yote yameelekezwa kuona jinsi Wabahrain watakavyohuisha msimu wa maombolezo ya Husseini ambapo Waislamu wengi na Mashia wa Ahlul-Bayt as wanausubiri kwa hamu. Bahrain inapoitwa kuwa “Karbala ya Pili”, basi tukio hili la huzuni, ambalo maelfu ya Wabahrain hulifanyia maandalizi kwa muda wa miezi miwili mfululizo kila mwaka, bila shaka litakuwa kitovu cha uangalizi wa wachunguzi, hususan wale wanaojali masuala ya Waislamu.

Sifa maalumu ya mwaka huu inatokana na vita vya wazi dhidi ya Mashia, utambulisho wao, itikadi zao na alama zao za kidini. Hali hii inakwenda sambamba na dalili za nia mbaya na juhudi za kuweka vikwazo vinavyolenga mipango na maonesho ya maombolezo ya Husseini, kwa mujibu wa taarifa za karibuni, tangu siku ya shahada ya Imam Jawad (as), imeamriwa kwamba alama za kidini zibaki ndani ya Husseiniyya na vituo vya maombolezo pekee, bila kuwekwa mitaani, pasi na sababu yoyote ya msingi, hapo ndipo kiini cha suala hili kilipo, lengo ni kubadilisha sura ya maombolezo ya asili na ya kawaida ya Wabahrain na kupunguza wigo wa mazingira ya kufanyika kwake, hii ina maana kwamba Muharram ijayo itakuwa mtihani wa kweli wa kiwango cha uthabiti na kushikamana kwa wapenzi wa Ahlul-Bayt (as) na alama zao, bila kujali ukubwa wa changamoto na hatari zilizopo.

Kwa sababu hiyo, kaulimbiu kuu ambayo wanazuoni wa Bahrain wameitangaza kwenye Muharram 1448 ni:

«لا معبود سِواك»

(Hakuna anayeabudiwa isipokuwa Wewe.)

Kaulimbiu hii iko wazi katika lengo lake; nayo ni kuzingatia itikadi ya Tawhid kama mhimili mkuu wa nyanja zote za harakati za mageuzi katika Umma wa Kiislamu, na kuimarisha imani ya kukataa aina yoyote ya utumwa kwa asiye Mwenyezi Mungu Mtukufu; iwe katika kiwango cha nafsi na matamanio yake, au katika kiwango cha kijamii na sanamu zilizotengenezwa na wanadamu katika sura zake zote za kale na za kisasa. Aidha, kaulimbiu hii inalenga kuimarisha roho ya kujiegemeza kwenye nguvu kamili ya Mola, kumtegemea katika shida na raha, kumtumainia katika neema na mitihani, kumwamini Yeye ambaye hana mshirika, na kuwa na yakini juu ya msaada na nusura Yake.

Kwa mujibu wa wanazuoni, lengo muhimu zaidi la kuchagua anuani hii kwenye Muharram ya mwaka huu ni kupuliza roho ya subira ya kimkakati na uimara katika kukabiliana na matatizo, njia ya haki haikosi miiba na vikwazo, na sunnah ya Mwenyezi Mungu kwa wale wanaofanya mageuzi ni kwamba hupitia majaribu, Qur’ani Tukufu na mwenendo wa Imam Hussein (as) vinatufundisha kwamba; subira haimaanishi kujisalimisha, bali ni uthabiti wenye busara na azma thabiti inayogeuza mateso kuwa neema na dhiki kuwa faraja.

Katika mwanga wa mtazamo huu, jambo lililo wazi ni kwamba; Muharram ya mwaka huu itageuka kuwa kituo cha kiroho, kitamaduni na kimaanawi kwa taifa linalotaka kuhifadhi utambulisho wake wa kidini wa asili mbele ya mamlaka inayojaribu kuubadili na kuujenga upya kulingana na mazingira yake ya kisiasa na kiusalama. Kwa hiyo, kila undani wa maombolezo ya Husseini yajayo utakuwa na maana kubwa; kuanzia kiwango cha ushiriki wa wananchi, aina ya majlisi, uwepo wa bendera, misafara na alama ambazo daima zimekuwa sehemu ya kumbukumbu na dhamiri ya pamoja ya Wabahrain.

Wabahrain wanafahamu vyema kwamba; kuilenga Ashura hakujatenganishwa na kuulenga uwepo wa umma wa Mashia nchini humo, Husseiniyya zinapowekewa mzingiro, shinikizo dhidi ya wanazuoni, wahadhiri na waombolezaji linapoongezeka hadi kufikia kukamatwa kiholela, na vikwazo vinapowekwa dhidi ya alama za Ashura, basi lengo linakuwa zaidi ya suala la uratibu au hatua za kawaida za kiutawala.

Suala hili linahusiana na kiini cha hisia ya kuwa sehemu ya jamii pamoja na haki ya asili ya kuonesha itikadi, alama na utambulisho, kwa hiyo, kusisitiza kwa wananchi juu ya kuhuisha Ashura itakuwa ni ishara ya kusimama kidete juu ya haki hiyo na kutokukubali kuiacha, bila kujali kiwango cha shinikizo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha