Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya mwaliko wa Ayatullah A‘rafi, Mkurugenzi wa Hawza, kwa wananchi ili washiriki kwa roho ya Ashura katika mazishi ya Kiongozi wa Umma, Imam Khamenei (ra), ni kama ifuatavyo:
Bismillahir-Rahmanir-Rahim
﴿وَلاَ تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُواْ فِي سَبِيلِ اللّهِ أَمْوَاتاً بَلْ أَحْيَاء عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ﴾
“Wala msidhanie kwamba wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu; bali wapo ni hai na kwa Mola wao wanaruzukiwa.”
Kufa kishahidi nahodha wa Mapinduzi ya Kiislamu katikati ya mawimbi ya dhoruba na misukosuko, baada ya miaka mingi ya jihadi isiyochoka na ustahimilivu wa kupigiwa mfano katika njia ya haki na ukweli, ni msiba mkubwa kwa Umma wa Kiislamu na kwa wananchi watukufu wa Iran, na kumezijaza nyoyo za Waumini huzuni na majonzi.
Kwa hakika, kiongozi shahidi na mtukufu wa Mapinduzi alikuwa imara katika njia ya malengo na maadili ya Mapinduzi ya Kiislamu hadi pumzi yake ya mwisho, akajitoa mhanga kwa ajili ya wananchi na Iran. Na leo, baada ya kupatikana mazingira ya kufanyika kwa mazishi ya mwili wake mtukufu, ni wajibu wetu kuonesha ushiriki wa kishujaa katika tukio hili la kihistoria nafasi ya mpendwa huyo katika nyoyo za wananchi hawa watukufu.
Ushiriki wa makundi yote ya wananchi kote nchini unaonyesha mapenzi na mshikamano wa watu kwa Imam wao mpendwa na shahidi, jambo ambalo linaonekana wazi katika siku za maombolezo ya Aba Abdillah Al-Hussein (as), na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu litakuwa msingi wa harakati ya Ashura kwa ajili ya kuitukuza nafasi ya kiongozi wetu mpendwa na shahidi.
Mimi nawalingania wananchi wa makundi yote, wapenda njia ya Khomeini na Khamenei, na wote walioumia kwa msiba huu mkubwa, washiriki kwa wingi katika tukio hili adhimu ili waandike ukurasa wa dhahabu katika historia ya nchi hii.
Alireza A‘rafi
Mkurugenzi wa Hawza za Elimu ya Dini
Maelezo ya Ratiba ya Sherehe za Kuaga na Mazishi ya Imam Shahidi
Jumamosi tarehe 13 na Jumapili tarehe 14 Tir 1405 Shamsia, zinazolingana na tarehe 19 na 20 Muharram: Sherehe za kuaga mwili mtukufu zitafanyika katika Musala wa Imam Khomeini (q.s.) mjini Tehran.
Jumatatu tarehe 15 Tir 1405 Shamsia, inayolingana na tarehe 21 Muharram:
Sherehe za mazishi zitafanyika mjini Tehran.
Jumanne tarehe 16 Tir 1405 Shamsia, inayolingana na tarehe 22 Muharram: Sherehe za mazishi zitafanyika katika mji mtukufu wa Qum.
Jumatano tarehe 17 Tir 1405 Shamsia, inayolingana na tarehe 23 Muharram: Sherehe za mazishi zitafanyika nchini Iraq.
Alhamisi tarehe 18 Tir 1405 Shamsia, inayolingana na tarehe 24 Muharram na usiku wa shahada ya Imam Sajjad (as): Sherehe za mazishi zitafanyika katika mji mtukufu wa Mashhad, na maziko yatafanyika katika Haram tukufu ya Imam Ridha (as).
Agizo la Ayatullah A‘rafi la Kuhamasisha Uwezo na Nyenzo Zote za Hawza
Ayatullah A‘rafi, Mkurugenzi wa Hawza, pia katika waraka rasmi alioutuma kwa wasimamizi na wanachama wa Makao ya “Balagh Mubin”, Baraza la Manaibu na Wasimamizi wa Hawza, wakurugenzi wa mikoa na maeneo mbalimbali, pamoja na viongozi wa shule na vituo vya kielimu vya Hawza kote nchini, alitangaza kuundwa kwa Kamati ya Hawza ya Mazishi ya Imam Shahidi na kusisitiza umuhimu wa kuhamasisha uwezo na nyenzo zote za Hawza kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya kishindo ya Imam Khamenei (ra).
Maoni yako