Jumatatu 6 Julai 2026 - 11:00
Kushiriki katika Mwamko Mkubwa wa Mazishi ya Imam Shahidi ni Wajibu wa Kisheria na Kiimani/ Asisitiza Umuhimu wa Kudai Kisasi na Kulipiza Damu ya Kiongozi Shahidi

Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, amesema kuwa; kushiriki kwa heshima na kwa wingi katika mwamko mkubwa wa mazishi ya Imam Shahidi ni wajibu wa wazi wa kisheria na kiimani, na amesisitiza ulazima wa kudai kisasi na kulipiza damu ya Kiongozi Shahidi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A'rafi, Mkurugenzi wa Hawza, katika ujumbe wake wa kimkakati aliouelekeza kwa Umma mkubwa wa Kiislamu, taifa kubwa la Iran, wanazuoni na viongozi wa kidini, taasisi kuu za Hawza, Baraza la Manaibu na Wakurugenzi wa Hawza, wakurugenzi wa mikoa na kanda za Hawza, pamoja na wakurugenzi wa vituo na vyuo vya elimu ya dini kote nchini Iran, amesisitiza kwamba: Heshima ya Iran na Uislamu, pamoja na kudhalilika kwa maadui wa taifa na Umma wa Kiislamu, kunategemea ushiriki wa wananchi wenye uelewa na ari kubwa katika hafla za mazishi ya Imam Shahidi mwenye hadhi kubwa zitakazofanyika Tehran, Qom, Iraq na Mashhad Tukufu.

Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, katika ujumbe huu muhimu, ameeleza kuwa; kushiriki kwa heshima katika mwamko mkubwa wa mazishi ya Imam Shahidi ni wajibu wa wazi wa kisheria na kiimani, na amesisitiza ulazima wa kudai kisasi na kulipiza damu ya Kiongozi Shahidi.

Maandishi kamili ya ujumbe wa Ayatullah A'rafi ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Umma mkubwa wa Kiislamu, Taifa kubwa la Iran, Wanazuoni na viongozi wa kidini, Taasisi kuu za Hawza, Baraza la Manaibu na Wakurugenzi waheshimiwa, Wakurugenzi waheshimiwa wa mikoa na kanda, Wakurugenzi watukufu wa vituo na vyuo vya elimu ya dini kote nchini, Assalamu Alaikum, na pole kwa siku hizi za maombolezo.

Kwa mara nyingine tena, inasisitizwa kwamba hafla za kuuaga, kusindikiza, kuzika, pamoja na majlisi za hitima za Imam Shahidi (ra), ni kiungo kinachokamilisha mapambano ya uwanjani na mitaani, jihadi ya mataifa na mwamko wa Umma wa Kiislamu. Uzembe wowote katika jambo hili, kushindwa kushiriki kwa kiwango cha kitaifa, au kupuuza kudai kisasi na kulipiza damu ya Kiongozi Shahidi (ra) na mashahidi watukufu, mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Hadhrat Wali al-'Asr (arawahuna fidah), mbele ya Imam Khomeini Mkuu (ra) na mashahidi wa Uislamu, haukubaliki kamwe. Katika maeneo yote ya Iran na duniani kote, ni lazima ari ya Hussein (as) na mwamko wa kitaifa na wa kimataifa usimamishwe.

Heshima ya Iran na Uislamu, pamoja na kudhalilika kwa maadui wa taifa na Umma wa Kiislamu, kunategemea ushiriki wa wananchi wenye uelewa na ari kubwa katika hafla zitakazofanyika Tehran, Qom, Iraq na Mashhad Tukufu.

Taifa la Iran, taifa la Iraq, mataifa ya dunia, mhimili wa Muqawama na vijana wapendwa wanapaswa kusimama na kuunda taswira isiyo na mfano. Vyombo vyote vya habari na taasisi zote vinapaswa kusimama, na kila mtu ajione kuwa ni mpiganaji wa njia hii na ni chombo cha kueneza ujumbe huu wa heshima na mabadiliko makubwa ya kihistoria na ya ustaarabu. "Ni lazima tusimame." Jambo hili, kwa mujibu wa maelekezo ya Mar'ajii wakuu, wanazuoni mashuhuri na kwa mujibu wa misingi na kanuni za Sheria na Fiqhi, ni wajibu wa wazi, wa lazima na wa dhahiri wa kisheria na kiimani.

Kwa matumaini ya kushuhudia mwamko mkubwa katika tukio hili adhimu la kumuaga Kiongozi Shahidi (ra), kutoa bay'ah upya kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, na kwa matumaini ya ushindi wa haki dhidi ya batili duniani kote.

وَمَا النَّصرُ إِلّا مِن عِندِ اللَّهِ العَزیزِ الحَکیمِ

Alireza A'rafi
Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha