Jumanne 7 Julai 2026 - 10:10
Trump! Utaona kitakachotokea

Hawza/ Bango lililobebwa katika hafla ya kumuaga Kiongozi Shahidi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jijini Tehran, lilimuelekezea maneno haya Trump, anayefahamika kama mcheza kamari: "Utaona kitakachotokea."

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katikati ya umati mkubwa wa watu waliojitokeza barabarani kwa ajili ya kumuaga Kiongozi wao Shahidi, Hadhrat Ayatullah Khamenei, hasira na azma ya kulipiza kisasi kwa damu yake vilikuwa vimefikia kilele chake. Waliokuwa wakimuaga Kiongozi Shahidi, huku wakipeperusha bendera nyekundu za kisasi, walikuwa wakipaza sauti kaulimbiu ya "Mauti kwa Marekani", na walitaka kulipiziwa kisasi dhidi ya wauaji wa Kiongozi wao Shahidi.

Trump! Utaona kitakachotokea

Mahudhurio ya kishujaa ya wananchi wa Iran katika hafla ya kuuaga na kuusindikiza mwili wa Kiongozi Shahidi yalikuwa ni kielelezo cha roho ya mapambano ya muqawama na mshikamano wao thabiti kwa malengo na misingi ya Kiongozi huyo ambaye ataendelea kuwa hai milele katika nyoyo za watu; Kiongozi aliyekutana na Mola wake akiwa amekunja ngumi yake kwa uthabiti na azma.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha