Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Dmitry Medvedev, Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi, atashiriki katika hafla ya mazishi ya mwili mtukufu wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Shahidi Ayatullah Mkuu Sayyid Ali Khamenei, mjini Tehran. Habari hiyo imetangazwa na Kazem Jalali, Balozi wa Iran nchini Urusi, katika mahojiano yake na Shirika la Habari la ISNA.
Alisema: "Dmitry Medvedev, Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Urusi, ambaye pia ni Rais na Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, atahudhuria hafla ya kumuaga Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Tehran kama mwakilishi maalumu wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin."
Jalali pia aliongeza kuwa; ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, wawakilishi wa Kanisa la Orthodox la Urusi, kundi la Muftii wa Kisunni wa Urusi pamoja na baadhi ya maulamaa wa Kishia wa nchi hiyo pia watashiriki katika hafla hiyo.
Kwa mujibu wa Jalali, ushiriki wa viongozi wa kisiasa na wa kidini wa Urusi katika hafla hiyo unaonesha "kina cha uhusiano na mafungamano yaliyopo kati ya Iran na Urusi."
Maoni yako