Jumatano 1 Julai 2026 - 11:22
Ujumbe Muhimu wa Ushiriki wa Wairaqi Katika Mazishi ya Imam Shahidi, Khamenei (ra)

Hawza / Mwandishi wa Kiiraqi, Muhammad Sadiq Al-Hashimi, ameandika: Mazishi makubwa yatakayoshuhudiwa kutoka kwa Mashia wa Iraq yanamaanisha uaminifu kwa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa njia ya Ahlul-Bayt (as), kwa Mara'jii wakubwa na kwa Hawza za Kielimu.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, katika kuelekea mazishi ya mamilioni ya watu ya Imam Shahidi Khamenei (ra), Mashia wa Iraq wanajiandaa kwa ajili ya kuupokea kwa heshima kubwa mwili mtukufu wa Marjii Mkuu wa Kishia, ili kutoa heshima kwa kiongozi shahidi wa Umma.

Makundi mbalimbali ya jamii ya Iraq, wakiwemo Mashia, viongozi wa makabila, wanazuoni wa dini, waombolezaji wa Ahlul-Bayt (as), watu mashuhuri wa Iraq pamoja na makundi ya Muqawama ya Iraq, yametangaza utayari wao wa kushiriki katika mazishi hayo makubwa.

Sherehe hii adhimu inabeba ujumbe muhimu kwa marafiki na maadui wa taifa la Iraq, katika muktadha huo, mwandishi wa Kiiraqi Muhammad Sadiq Al-Hashimi ameandika makala ifuatayo:

Watu huru wa Iraq, kwa uwezo wao wote, nguvu yao ya kijamii na imani yao thabiti, watashiriki katika mazishi na kutoa mkono wa pole kwa Imam Shahidi, Imam Khamenei (ra), pamoja na familia yake tukufu, maana muhimu zaidi ya mazishi haya nchini Iraq ni kama ifuatazo:

1. Mashia wa Iraq katika historia yote daima wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa nusra, kufanya jihadi na kuweka misimamo ya heshima. Katika hatua hii nyeti ya kihistoria ya kipindi cha jihadi pia, bila shaka watakuwa mstari wa mbele kwa ushiriki wenye uelewa na utambuzi, hili ndilo jambo dogo kabisa tunaloweza kulifanya kwa uaminifu wetu kwa dini na kama maandamano dhidi ya uhalifu mkubwa wa Marekani dhidi ya Marajii; uhalifu wa wazi dhidi ya Hawza na Marajii, ambao unapaswa kujibiwa kwa sauti kubwa ya Mashia ya kuulaani, na taifa la Iraq pia lina wajibu wa kushiriki katika wito huu wa kweli.

2. Mazishi makubwa yatakayoshuhudiwa kutoka kwa Mashia wa Iraq yanamaanisha uaminifu kwa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa njia ya Ahlul-Bayt (as), kwa Marajii wakubwa na kwa Hawza za Kielimu. Vilevile, ushiriki mkubwa katika mazishi haya unaonesha kwamba; Mashia wanamiliki uelewa, utambuzi na maandalizi yanayohitajika kwa ajili ya kuyatetea madhehebu yao, Marajii wao, mchakato wao wa kisiasa na haki zao za kikatiba dhidi ya uchokozi. Zaidi ya hayo, kushiriki katika hafla hii kunamaanisha kuunga mkono Mapinduzi ya Kiislamu; mapinduzi ambayo yanawalinda Waislamu kwa ujumla na yanapigania dini na maadili dhidi ya uchokozi wa makafiri.

3. Mazishi makubwa yanamaanisha kwamba: Umma wa Kishia unatuma ujumbe wake kwa Marekani; ujumbe wa kulaani matendo yao, kukataa roho yao ya kiburi na ubeberu, na kulaani uhalifu wao. Muhimu zaidi kuliko yote, taifa la Iraq kupitia ushiriki huu linatangaza kupinga uvamizi na ukaliaji wa mabavu, na linataka mamlaka kamili ya kitaifa pamoja na uhuru.

Vilevile, taifa la Iraq katika mazishi haya litapata fursa kubwa ya kulaani uhalifu wa Uingereza na Marekani dhidi ya Mashia wa Iraq katika kipindi chote cha karne ya ishirini na miaka iliyofuata, pamoja na uhalifu wa utawala wa Kizayuni dhidi ya mashujaa wa Hashd al-Shaabi na watu wengine huru miongoni mwa wana wa ardhi hii.

4. Mazishi makubwa yanamaanisha kwamba Mashia wa Iraq, kwa uelewa, ushiriki mpana na wa dhati, wanaandika uwepo wao katika vita vya hatima, na mbele ya aina yoyote ya uchokozi kutoka katika mazingira ya kimataifa na ya kikanda, wanathibitisha uwepo wao, utambuzi wao na nguvu yao.

5. Mazishi makubwa yanaondoa mipaka ya kijiografia na kuugeuza Umma wa Kishia kuwa Umma mmoja wenye bendera moja. Hasa kwa kuwa adui anataka kutugawa vipandevipande na kutusambaratisha ili iwe rahisi kwake kuliangamiza taifa letu na nguvu zetu, ilhali sisi sote tuko ndani ya jahazi moja; jahazi la heshima na la kuutetea Uislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha