Jumatatu 29 Juni 2026 - 21:33
Ujumbe Muhimu wa Ayatullah A'rafi kuwaelekea Wabebaji Ujumbe wa Dini/ Asisitiza Kufafanua Umuhimu wa Matumizi Bora na Kuepuka Ubadhirifu

Hawza/ Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, ameeleza kuwa; kueneza na kuimarisha utamaduni wa “usimamizi bora wa rasilimali” na “matumizi yenye uwajibikaji” ni miongoni mwa vielelezo muhimu vya jihadi ya zama hizi, na amewapa jukumu wahubiri na watoa mawaidha la kuwafafanulia wananchi umuhimu na ulazima wa kuweka mipaka katika matumizi na kujiepusha na ubadhirifu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini kamili ya ujumbe wa Ayatullah Alireza A'rafi, Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, uliotolewa kwa wanazuoni wa dini, makhatibu na wahubiri ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Wanazuoni waheshimiwa, makhatibu watukufu na wahubiri mashuhuri wa ujumbe wa Karbala (Mwenyezi Mungu aendelee kuuhifadhi utukufu wenu).

Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh

Kwa sasa tupo katika mwezi wa Muharram, mwezi wa kuhuisha maadili ya Mwenyezi Mungu na kubainisha mafundisho adhimu ya Ahlul-Bayt (as), Muharram ni msimu wa kuongeza uono wa ndani (basira) na kuimarisha uhusiano kati ya “busara ya kidini” na “maslahi ya Umma wa Kiislamu.”

Leo hii, wakati ambapo kambi ya ubeberu ikiongozwa na Marekani pamoja na utawala wa Kizayuni unaoikalia kwa mabavu Quds, imeelekeza vita vya mchanganyiko na vya pande zote dhidi ya azma ya taifa tukufu la Iran, jukumu la wanazuoni wa dini katika kubainisha vipengele vya “Jihadi ya Ufafanuzi” na “mapambano katika uwanja wa jihadi” limeongezeka maradufu.

Miongoni mwa vielelezo muhimu vya jihadi ya leo ni kueneza na kuimarisha utamaduni wa “usimamizi wa rasilimali” na “matumizi yenye uwajibikaji.” Kuweka matumizi katika mipaka na kujiepusha na ubadhirifu kunamaanisha kutumia rasilimali kwa hekima na ufanisi bila kuvuka mipaka ya wastani. Qur'ani Tukufu imetukataza kwa kauli kali kabisa kufanya ubadhirifu na matumizi ya hovyo:

﴿إِنَّ الْمُبَذِّرِينَ كَانُوا إِخْوَانَ الشَّيَاطِينِ﴾

(Israa: 27)

Katika njia hii, kielelezo chetu cha vitendo daima ni mwenendo wenye hekima wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei (q.s.), ambaye siku zote alisisitiza kwa namna ya pekee umuhimu wa “mtindo wa maisha usio na ubadhirifu” na “kutumia kwa kiwango cha juu kabisa rasilimali za nchi.” Bila shaka, leo pia Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei (Mwenyezi Mungu aendelee kuhifadhi baraka zake), akiwa kiongozi wa Mfumo wa Kiislamu na mwendelezaji wa njia hiyo yenye nuru, anatarajia jamii ya kimapinduzi, kwa kutegemea utamaduni wa kuridhika na kile kilichopo (qana'a) pamoja na kurekebisha mfumo wa matumizi, imkwamishe adui katika kufanikisha malengo yake ya vita vya kiuchumi.

Kutoka kwenu, maafisa wa vita laini na walinzi wa mimbari na mihrabu, kunatarajiwa kwamba katika majlisi zenye hamasa za maombolezo, mkitumia mafundisho yenye nuru ya Ahlul-Bayt (as), myape umuhimu wa pekee maeneo haya matatu muhimu na myafafanue kwa wananchi:

1- Usimamizi wa matumizi ya maji:
Maji ni amana ya Mwenyezi Mungu na ndiyo chanzo cha uhai. Katika mazingira ya sasa, kuweka matumizi ya maji katika mipaka ni mfano wa kushirikiana katika wema na uchamungu:

﴿تَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى﴾.

2- Usimamizi wa matumizi ya nishati:
Nishati ni nguzo ya nguvu ya uchumi na usalama wa taifa. Matumizi bora ya umeme na mafuta ni mwitikio kwa wito wa kujitegemea na ni namna ya kukabiliana na vita vya kiuchumi vya adui. Kuwapa watu elimu kuhusu kuepuka upotevu wa nishati ni miongoni mwa majukumu ya uelimishaji kwa wahubiri wapendwa.

3- Usimamizi wa matumizi ya plastiki:
Uchafuzi wa mazingira ni miongoni mwa mifano ya kufanya uharibifu duniani. Kueneza mtindo wa maisha unaolinda mazingira na kutumia mbinu mbadala zilizo safi ni miongoni mwa njia za kuhifadhi afya ya jamii na kutekeleza haki ya vizazi vijavyo.

Wahubiri waheshimiwa wanapaswa katika vipindi mbalimbali vya programu na maombolezo ya Muharram na Safar ya Hussein, kuwahimiza wananchi kuelekea “kheri ya wote” na “kulinda rasilimali na mali za taifa.” Bila shaka, kuweka matumizi katika mipaka katika nyanja hizi tatu ni nguzo ya usalama wa taifa na ni ishara ya ukomavu wa kiimani wa jamii yetu.

Tunatumaini kwamba kwa fadhila za Hadhrat Baqiyyatullah Al-A'dham (arwahuna lahul-fida), na kwa kupata msukumo kutoka katika madrasah ya Ashura na Arubaini, msimu huu wa maombolezo ya Imam Hussein (as) utakuwa sababu ya ustawi na maendeleo ya kimwili na kiroho kwa taifa shujaa la Iran.

Alireza A'rafi
Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha