Jumapili 12 Julai 2026 - 12:50
Mazishi ya Mwili wa Imam Khamenei nchini Iraq na Iran Yalikuwa Ni Kuhuisha Bai'a na Tangazo la Msimamo wa Kidini na Kisiasa

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi amesema: "Kwa kufanyika mazishi ya mwili wa Shahidi Imam Khamenei nchini Iraq na Iran, kambi ya haki ilipata ushindi katika kiwango cha maoni ya umma duniani, huku ubeberu wa dunia ukishindwa."

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika khutba za Swala ya Ijumaa alizozitoa katika Husseinia al-A'dham Fatimiyyah mjini Najaf Ashraf, alisema:

"Ni kwa namna gani mazishi ya mwili wa ‘Sayyid al-Wali’, Shahidi Imam Khamenei, nchini Iraq na Iran yaligeuka kuwa tukio la kisiasa katika kiwango cha Iraq, Iran na dunia? Kambi ya haki ilipata ushindi katika kiwango cha maoni ya umma duniani, huku ubeberu wa dunia ukishindwa."

Aliongeza kuwa; mazishi hayo hayakuwa tu hafla ya maziko, bali ilikuwa ni kuhuisha bai'a, ahadi na kiapo cha uaminifu; hayakuwa mazishi ya kawaida, bali lilikuwa tamko la msimamo wa kidini na kisiasa; hayakuwa mazishi ya kawaida, bali ilikuwa udhihirisho wa utambulisho; na hayakuwa mazishi ya kawaida, bali ulikuwa ujumbe wa umoja wa mataifa yaliyodhulumiwa dhidi ya ubeberu wa dunia.

Alisema kuwa; makadirio yanaonesha kuwa watu kati ya milioni 8 hadi 10 walishiriki katika mazishi yaliyofanyika Najaf Ashraf na Karbala.

Aidha alisema: "Hapa tunapaswa kulishukuru taifa la Iraq lililo waaminifu, na kuliambia taifa letu kwamba mmetuinua vichwa vyetu kwa heshima; Mwenyezi Mungu awainue duniani na Akhera. Pia tunapaswa kuzishukuru taasisi za usalama na serikali, Atabaat Tukufu pamoja na Hawza. Iraq sasa inachora ramani mpya ya mustakabali wake, na dau lililowekwa kwamba mwelekeo wa utaifa ungeushinda mwelekeo wa kidini limefeli."

Kampeni ya "Fajr" na Kufichuliwa kwa Mafaili ya Ufisadi

Akizungumzia masuala ya ndani ya Iraq alisema: "Kampeni ya 'Fajr' pamoja na kufichuliwa kwa mafaili ya ufisadi imepokelewa kwa matumaini na mtazamo chanya na wananchi wa Iraq. Hata hivyo, leo kuna pendekezo la kutoa msamaha kwa wezi kwa sharti la kurejesha mali walizoiba. Tunaamini kuwa mradi huu unamaanisha kuwahamasisha kufanya wizi tena."

Alisisitiza kuwa; vyombo vya mahakama vinapaswa kuwafanyia wahusika hao ukaguzi kwa haki na kwa msimamo thabiti, na kwamba kushughulikia suala hilo kunapaswa kufanyika bila kuathiriwa na maagizo au mashinikizo ya ndani wala ya nchi jirani.

Aliongeza kuwa; kila mtu anapaswa kuunga mkono mradi wa "Kampeni ya Fajr", huku akionya dhidi ya kuuingiza katika siasa za makundi.

Kurejea kwa Ngoma za Vita kati ya Iran na Marekani

Akizungumzia masuala ya kimataifa alisema: "Ngoma za vita kati ya Iran na Marekani zimeanza kupigwa tena. Marekani imethibitisha kushindwa kwake katika medani ya kimataifa, kijeshi na hata ndani ya nchi yake, wakati Iran imethibitisha nguvu zake za kijeshi, kisiasa na uungwaji mkono wa wananchi wake."

Aliongeza kuwa; leo taifa la Iran linapaza sauti ya "kisasi", na fatwa mbalimbali zimetolewa zikieleza kuwa damu ya wauaji wa "Sayyid al-Wali" ni halali. Aidha alisema kuwa leo taifa la Iran limeuweka ulimwengu mbele ya hali mpya yenye ujumbe kwamba: "Muuaji hataweza kuikimbia mikono ya haki."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha