Jumapili 12 Julai 2026 - 15:30
Kutoka Ndoto za Kuuporomosha Mfumo Hadi Uhalisia wa Uimara Wake; Historia Yawapa Somo Wapinzani wa Iran

Hawza/ Historia daima hutenganisha ukweli na dhana. Wanasiasa kama Lindsey Graham, kwa mahesabu yasiyo sahihi na utabiri usio na msingi, walikuwa wakiahidi kuporomoka kwa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hata hivyo, kupita kwa muda kumedhihirisha kuwa wale waliodai mfumo huo ungeanguka, wao wenyewe ndio waliosahaulika, kwa upande mwingine, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa kutegemea damu ya mashahidi na irada ya wananchi wake, si tu kwamba imesalia imara, bali sasa baada ya kupita karibu miongo mitano, inatambulika kama moja ya nguzo zenye nguvu duniani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni simulizi iliyojaa misukosuko ya mapambano, uthabiti na ushindi dhidi ya njama na hila mbalimbali za maadui walioapa kuuangamiza mfumo huo. Tangu siku za mwanzo za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ubeberu wa kimataifa na washirika wake wa kikanda walitumia uwezo wao wote katika juhudi za kuupindua Mfumo mpya wa Jamhuri ya Kiislamu. Vita vya kulazimishwa vya miaka minane, vikwazo vikali vya kiuchumi, kuunga mkono makundi ya kigaidi na ya kujitenga, pamoja na kampeni kubwa za propaganda za vyombo vya habari, ni sehemu tu ya mashambulizi hayo yaliyopangwa. Hata hivyo, hakuna hata moja ya njama hizo iliyofanikiwa badala yake Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, chini ya uongozi wa kimungu na kwa kutegemea azma ya kitaifa, ilitoka katika kila hatua ikiwa imara zaidi, na kwa karibu miongo mitano imeendelea kuthibitisha uthabiti wake.

Katika mkondo wa historia, daima kumekuwepo na mvutano kati ya nguvu za mpito na ukweli wa kudumu. Lindsey Graham – moja ya nyuso zilizokuwa zikionekana mara kwa mara katika vyombo vya habari vya Magharibi kwa mashambulizi makali dhidi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran – alikuwa mfano wa mkondo huo wa misimamo ya kihisia ambao kwa utabiri usio na msingi uliendelea kutangaza kuporomoka kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hata hivyo, sasa, wakati yeye ameondolewa katika medani ya dunia kutokana na kifo cha ghafla na kutupwa katika jalala la historia, si tu kwamba kuporomoka kule alikokuwa akudai hakujatokea, bali mamlaka na nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesalia imara zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Historia imeonesha kuwa nguvu za uongo na uchambuzi wa kihisia ni vivuli vya muda mfupi vinavyotoweka mbele ya jua la ukweli. Wanasiasa na wachambuzi wengi wa Marekani waliokuwa wakitumia lugha hiyo hiyo ya vitisho na kutabiri kuanguka kwa Mfumo wa Iran, leo hawakumbukwi tena. Waliondoka pamoja na ahadi zao za ushindi usioepukika zikazikwa pamoja nao, ilhali Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haikuvuka tu njama zote, bali kila changamoto mpya ilizidi kuifanya ijitayarishe na kuimarisha uwezo wake wa kukabiliana na misukosuko ya kimataifa.

Tofauti hii iliyo wazi kati ya "kifo cha utabiri wa maadui" na "uhai wenye utukufu wa Mfumo wa Kiislamu" ni ushahidi kwamba nguvu ya kweli haipo katika maneno yenye makelele ya wanasiasa wa Magharibi, bali imo katika irada ya pamoja ya taifa lililojengwa juu ya msingi wa imani na malengo ya Mwenyezi Mungu.

Lindsey Graham na wale wenye mtazamo kama wake, katika juhudi zao zisizo na mafanikio za kuudhoofisha Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, wameishia kuthibitisha uimara na mizizi yake imara. Kwa sababu, kadiri adui anavyozidi kutembea kwenye ukingo wa vitisho, ndivyo uimara wa mfumo huu unavyozidi kuvunja kila dhana ya kuporomoka kwake.

Leo, baada ya kupita kwa muda, imebainika kwamba wale waliokuwa wakitangaza kuanguka kwa Mfumo Mtukufu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wao wenyewe wameangukia katika mtego wa kuporomoka na kusahaulika, au wataangukia humo. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran bado imesimama imara kama moja ya nguzo zenye nguvu duniani; si kwa sababu ya madai ya kisiasa, bali kutokana na kusimama katika njia ya haki na kupambana na dhulma chini ya kivuli cha ahadi za Mwenyezi Mungu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha