Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia wa Pakistan, katika kauli zake huku akielezea wasiwasi mkubwa juu ya matukio ya hivi karibuni katika eneo, alitahadharisha dhidi ya hatua yoyote ya kijeshi na ya kivamizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na akasisitiza kuwa: shambulio lolote la kibeberu dhidi ya Iran litakuwa kosa kubwa na lenye gharama kubwa.
Aliendelea kwa kurejelea mafungamano ya kina ya kidini, kitamaduni na kihistoria kati ya mataifa mawili ya Iran na Pakistan, akasema: kama tulivyoshuhudia pia hapo awali, katika hali ngumu na nyeti, mataifa ya Iran na Pakistan daima yamesimama pamoja, na leo pia mshikamano huo unaonekana waziwazi.
Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Pakistani aliongeza kuwa: hali ya sasa, kuliko wakati mwingine wowote, inahitaji umoja wa Umma wa Kiislamu na msimamo wa pamoja dhidi ya njama na hila za nguvu za kibeberu.
Katika mwendelezo wa hotuba yake, akiashiria juhudi za hivi karibuni za nguvu za kiutawala dhidi ya Iran, alisisitiza kuwa: awamu ya kwanza ya mashambulizi ya kibeberu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran—yaliyolenga kuunda shinikizo la kijamii, kuchochea maoni ya umma dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na mfumo wa dola, kueneza vurugu na ukosefu wa usalama, na kuwalenga watu mashuhuri—kwa fadhila za Mwenyezi Mungu ilishindwa kabisa.
Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia wa Pakistan alionya kuwa: iwapo nguvu za kibeberu katika awamu ya pili, badala ya mashinikizo ya kisiasa na kisaikolojia, itakimbilia chaguo la kijeshi na kulazimisha vita, bila shaka kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, madhalimu hawa watakabiliwa na kushindwa kwa kihistoria na funzo kubwa.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, sambamba na kumuombea afya njema na umri mrefu Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Mtukufu Ayatollah Mkuu Sayyid Ali Khamenei, pamoja na kudumishwa usalama wa Jamhuri ya Kiislamu na taifa la Iran, alisema: Insha’Allah, chini ya uongozi wa hekima wa Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, wakati wa kiburi, majivuno, udhalimu na tamaa ya kutawala itafikia tamati, na kipindi hiki kitakuwa mwanzo wa ushindi wa Uislamu, heshima ya Iran, na kusambaratika kwa ubeberu wa kimataifa.
Maoni yako