Ijumaa 30 Januari 2026 - 20:46
Trump mpumbavu haijui Jamhuri ya Kiislamu ya Iran/ Kuishambulia Iran kutasababisha mlipuko wa volkano katika ukanda

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Al-Haidari alisema: Trump mpumbavu haijui Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, halijui taifa la Iran lenye kujihami na lenye imani; hamjui Kiongozi Mkuu wa Kiislamu (Waliyyu-l-Faqih) ni nani wala maana ya Waliyyu-l-Faqih ni ipi. Haelewi kwamba endapo atathubutu kuishambulia Jamhuri ya Kiislamu, ni hatima gani iliyojaa aibu, uharibifu, udhalili na kushindwa inayomsubiri.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hashim Al-Haidari, Katibu Mkuu wa Harakati ya Ahdullah Iraq, katika taarifa yake huku akijibu kauli za hivi karibuni za Trump kuhusu Jamhuri ya Kiislamu, alisema: Trump mpumbavu haijui Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, halijui taifa la Iran lililo na mujaahidina na lenye imani; hamjui Kiongozi Mkuu wa Kiislamu (Waliyyu-l-Faqih) ni nani wala maana ya Waliyyu-l-Faqih ni ipi. Haelewi kwamba endapo ataivamia Jamhuri ya Kiislamu, ni hatima gani iliyojaa aibu, uharibifu, udhalili na kushindwa itakayomsubiri.

Matini kamili ya taarifa hii ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:


﴿وَلَا تَهِنُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَنْتُمُ الْأَعْلَوْنَ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ﴾


“Msilegee wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu ikiwa mtaendelea kuwa waumini.”

Tena na tena, Trump kwa fikra zake, maamuzi yake na mienendo yake, amethibitisha kuwa ni mtu asiye na haya, duni, mchafu na mwovu. Yeye ni doa la aibu kwenye paji la uso wa mfumo potovu wa kisiasa wa Marekani; bali atakuwa doa la aibu kwa Wamarekani endapo watanyamaza mbele yake na kumwacha aendelee kubaki madarakani.

Trump mpumbavu haijui Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, halijui taifa la Iran lililo lenye imani; hamjui Kiongozi Mkuu wa Kiislamu ni nani wala maana ya Kiongozi Mkuu wa Kiislamu ni ipi. Haelewi kwamba endapo atathubutu kuivamia Jamhuri ya Kiislamu, ni hatima gani iliyojaa aibu, uharibifu, udhalili na kushindwa inayomsubiri. Hapo ndipo ataiona volkano itakayolipuka katika eneo zima dhidi yake na dhidi ya chembechembe za uasi, ufisadi na dhulma, yaani Israel inayoelekea kuangamia (Insha’Allah).

Trump duni, mwana wa duni, haelewi wala hajui—hata kwa kiwango cha kichwa cha sindano—maana ya aya:


﴿إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ﴾

“Mkimnusuru Mwenyezi Mungu, Naye atawanusuru,”


wala haelewi maana ya uwepo wa mamilioni ya watu waliopagawa na mapenzi ya shahada, kujitoa mhanga na jihadi, ndani ya Iran ya Kiislamu na nje yake; watu wanaosubiri ishara na wakati wa kisheria ili kuzigeuza balozi zote na kambi zote za Marekani katika eneo hili kuwa Jahannamu, na kumlenga kila Mmarekani aliyepo katika eneo letu.

Uasi wa Kimarekani wa Trump leo umezikumba nchi zote za eneo na mataifa yake; ikiwemo Iraq, Lebanon, Palestina na nchi nyingine. Bila shaka, mataifa huru na yenye heshima ya eneo hili hayatainamisha vichwa vyao mbele ya uasi huu, uingiliaji huu na maagizo ya waziwazi.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:


﴿سَيُهْزَمُ الْجَمْعُ وَيُوَلُّونَ الدُّبُرَ﴾

“Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma..”

Sayyid Hashim Al-Haidari

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha