Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika kilele cha makabiliano kati ya haki na batili ambapo maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wanakusudia kukabiliana nayo kwa kila aina ya hila za kishetani, “Baraza la Maulamaa wa Najaf Ashraf” kwa kutoa tamko, limetangaza upya ahadi yake kwa mfumo huu mtukufu chini ya uongozi wa busara wa Mtukufu Ayatollah Khamenei.
Tarjama ya matini ya tamko ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
(وَلَقَدْ كَتَبْنَا فِي الزَّبُورِ مِن بَعْدِ الذِّكْرِ أَنَّ الْأَرْضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ الصَّالِحُونَ)
Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu ya kwamba, nchi watairithi waja wangu walio wema.
(Al-Anbiyaa: 105)
Katika nyakati hizi za kihistoria ambapo mapambano kati ya kambi ya haki na kambi ya ubeberu wa kimataifa yamezidi kushika kasi, na adui ametutaka tuchague moja kati ya mawili: “kukabiliana nae au udhalili”, “Baraza la Maulamaa wa Najaf Ashraf”, kwa kauli mbiu ya “Hayhata minna dh-dhillah” (uwe mbali nasi udhalili), linatangaza upya ahadi yake kwa “ngome ya mwisho” na chemchemi ya heshima na utu, yaani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; mfumo uliosimama juu ya “utawala wa faqihi” na unaoendeshwa chini ya uongozi wa busara wa Ayatollah Khamenei (roho zetu ziwe fidia kwake). Sisi katika baraza hili, tunaona kushikamana na “utawala wa faqihi” si msimamo wa kisiasa wa mpito, bali ni ahadi ya kisheria inayotokana na imani; kwa sababu utawala huu ni hifadhi ya Ushia na Waislamu; kama ilivyokuja katika riwaya tukufu: “Qum ni kiota cha Ahlul-Bayt wa Muhammad (s.a.ww) na ni hifadhi ya Mashia wetu”; na [pia imeelezwa kuwa mji huo] ni uwanja wa maandalizi ya harakati ya kusimamisha mapinduzi matukufu ya Bwana wetu, Sahib az-Zaman (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake).
Katika muktadha huu tunatangaza kwamba: shambulio lolote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu—iwe ni kwa njia ya vita laini au mashinikizo ya kiuchumi—linamaanisha kulenga nguzo ya hema na kuwaweka hatarini watu wote huru wa dunia; na sisi tunaona uhai wetu, utambulisho wetu na heshima yetu kuwa vimefungamana na uhai wake. Kwa hivyo, tutaweka rasilimali zetu zote za kimada na kiroho chini ya bendera ya kiongozi wake ambaye ni “Hussein wa zama”, na katika mwelekeo wa kumtetea.

Pia, tunalipongeza taifa la Iran na makamanda wa nchi hiyo kwa msimamo wao wa kishujaa; msimamo unaothibitisha kila siku kuwa “fadhila ya Mwenyezi Mungu” ndiyo inayosimamia uendeshaji wa uwanja wa muqawama, na inaonesha kwamba, hatimaye azma ya waliodhulumiwa itashinda. Kwa msingi huo, tunaualika umati wa watu wetu, wawe macho na waangalifu, wajiepushe na “sumu ya vyombo vya habari” ambayo lengo lake ni kukata uhusiano na kituo cha Wilaya; na tunasisitiza kuwa; busara ni kutohakikisha kwamba; hatuwezi kuwa mshale katika upinde wa maadui wa Mwenyezi Mungu unaopigwa kuelekea mshipa mkuu wa Wilaya.
Iran itabaki yenye fahari, na Waliyyu-l-Faqih atabaki kuwa taa ya uongofu itakayotuongoza katika giza la fitna; na mashinikizo hayatatuongezea chochote isipokuwa kuimarisha zaidi kushikamana kwetu na “kamba imara ya Mwenyezi Mungu”.
(إِنَّ اللَّهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا)
Baraza la Maulamaa wa Najaf Ashraf
Maoni yako