Ijumaa 23 Januari 2026 - 23:30
Kutishia kumuua Ayatollah udhma Khamenei ni njama ya kishetani; makelele ya Trump hayadumu na hatima yake ni pipa la taka la historia

Hawza/ Harakati ya Amali ya Kiislamu ya Lebanon, kwa kulaani vikali vitisho vya Donald Trump dhidi ya Ayatollah Khamenei, ilisema hatua hiyo kuwa ni njama ya kishetani na uonevu wa Kimarekani-Kizayuni, na ikasisitiza kuwa makelele na vitisho vya Trump hayatadumu, na hatima ya madhalimu hawa ni pipa la taka la historia.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Harakati ya Amal ya Kiislamu ya Lebanon ilitoa tamko kali huku ikilaani vitisho vya Rais wa Marekani dhidi ya Mtukufu Ayatollah Khamenei, Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kusema kuwa ni njama ya kishetani pamoja na uonevu wa chuki wa Kimarekani-Trump na Kizayuni.

Katika tamko hilo, kwa kurejelea kauli za hivi karibuni za Donald Trump, aliyesema kwamba “ikiwa Iran itafanya jambo lolote, nitaifuta kabisa kutoka juu ya uso wa dunia”, ilisisitizwa kuwa leo mbele ya macho na masikio ya ulimwengu mzima, ni Marekani na kiumbe wake aliyemlea—utawala haramu na wa kihalifu wa Kizayuni—wanaotekeleza uhalifu ndani na nje ya mipaka.

Chama hiki cha kisiasa kilionesha mshangao wake mkubwa juu ya ukimya wa dunia dhidi ya matendo na kauli za Trump, na kikakumbusha mifano kama vile vitisho vyake vya wazi vya kuivamia Greenland, kumteka nyara Rais wa Venezuela pamoja na mke wake, kupora mafuta na utajiri wa nchi hiyo, pamoja na vitisho dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika sehemu nyingine ya tamko hilo, ilirejelewa kiburi na tamaa ya madaraka ya Trump mbele ya washirika wake wa Ulaya, ridhaa yake kwa mauaji ya kimbari huko Ghaza na uharibifu kamili wa eneo hilo kwa silaha za Marekani, kuwasha taa ya kijani kwa ajili ya kuangamiza kusini mwa Lebanon na juhudi za kung’oa kabisa Mhimili wa Kishujaa wa Muqawama nchini Lebanon, pamoja na kuweka vikwazo vya kiuchumi vinavyoilemaza nchi hiyo kwa lengo la kuilazimisha isalimu amri.

Harakati hiyo ilihitimisha tamko lake kwa kusisitiza kuwa makelele ya kikatili na uonevu wa Kimarekani-Kizayuni, pamoja na mienendo ya kigaidi, ya kiburi na ya aibu ya Trump, hayatadumu kwa muda mrefu. Ilibainisha wazi kuwa: hatima ya madhalimu na mashetani wa kihalifu ni pipa la taka la historia, na mataifa huru na yenye heshima yatawawajibisha na kuwafukuza wote walioichafua mikono yao kwa damu ya wasio na hatia.

Kutishia kumuua Ayatollah udhma Khamenei ni njama ya kishetani; makelele ya Trump hayadumu na hatima yake ni pipa la taka la historia

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha