Ijumaa 30 Januari 2026 - 00:30
Mradi wa Marekani na Israel ni kuondoa uhuru na muqawama katika eneo/ Vita vyovyote dhidi ya Iran vitahusisha eneo zima

Hawza/ Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon, katika mkusanyiko wa mshikamano wa Wale­banon na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alisisitiza kuwa Marekani na utawala wa Kizayuni wameilenga Lebanon, Ghaza, Syria na Iran ndani ya mradi mmoja wa kikoloni, na kwamba uvamizi wowote dhidi ya Iran utaingiza moja kwa moja Hezbollah na eneo zima katika mgogoro.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon, katika hotuba yake kwenye hafla ya mkusanyiko wa mshikamano wa Wale­banon na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akichora taswira ya vipengele vya mradi mmoja wa Kimarekani–Kizayuni, alisisitiza: Leo Marekani na utawala wa Kizayuni wanaitazama Lebanon, Ukanda wa Ghaza, Syria, Iran na eneo zima kama sehemu ya mradi mmoja wa kikoloni; mradi ambao lengo lake ni kuangamiza mpango wowote wa muqawama, uhuru na kusimama kidete katika eneo lote la eneo.

Akirejea harakati za kisiasa na kiusalama za miezi miwili iliyopita, alisema: Pande kadhaa na wapatanishi wameuliza kwa uwazi iwapo, endapo Marekani na Israel zitapigana vita dhidi ya Iran, Hezbollah itaingilia kati au la, na wamejaribu kuchukua ahadi kutoka kwa Hezbollah kwamba isiingie kwenye mapigano. Wapatanishi hawa wametangaza wazi kuwa Marekani na utawala wa Kizayuni wanachunguza matukio mbalimbali; yakiwemo kuishambulia kwanza Hezbollah kisha Iran, au kuishambulia kwanza Iran kisha Hezbollah, au kuzishambulia kwa wakati mmoja zote mbili. Katika matukio yote haya, Hezbollah iko ndani ya duara la vita, na adui anajaribu kuona iwapo anaweza kuzitenganisha nguvu hizi au la.

Katibu Mkuu wa Hezbollah aliongeza: Mbele ya uwezekano huu uliochangamana, na mbele ya uvamizi usiotofautisha, tunajiona tukiwa katikati ya mabadiliko na mashambulizi, na tumeazimia kujilinda. Jinsi ya kuchukua hatua—iwe ni kuingilia au kutoingilia—na maelezo yake yataamuliwa kulingana na hali ya uwanja na katika wakati unaofaa.

Akisisitiza kuwa Hezbollah si ya upande wa kati, alisema: Maelezo ya hatua yataamuliwa kwa mujibu wa uwanja wa vita na maslahi; na kutokuwapo kwa uwiano wa nguvu hakuondoi haki ya kujilinda, kwa sababu ulinzi—iwe katika hali ya kutokuwiana kwa nguvu au mbele ya uvamizi—ni kanuni ya msingi ya kuzuia kutimia kwa malengo ya adui.

Kutishia uongozi ni kutishia uthabiti wa eneo

Sheikh Naim Qassem, akirejea vitisho vilivyotolewa dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, alisisitiza: Hezbollah inaamini uongozi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kama kanuni ya imani na itikadi, na tishio lolote la kumdhuru—iwe kutoka kwa Trump au mtu mwingine yeyote—ni tishio dhidi ya mamilioni, hata makumi ya mamilioni ya watu, na haliwezi kupuuzwa.

Alisema kuwa: Wajibu wa kiimani na kiitikadi wa watu wote ni kukabiliana na tishio hili, na Hezbollah inajiona imejitolea kuchukua tahadhari zote muhimu.
Katibu Mkuu wa Hezbollah alisisitiza: Kuuawa kwa njia ya hujuma, Mwenyezi Mungu aepushie mbali, kutakuwa sawa na kuua uthabiti wa eneo na hata wa dunia; na mbele ya tishio kama hilo, kuna mamlaka kamili ya kuchukua hatua yoyote inayofaa.

Kwa upande mwengine Sheikh Qassem, akijibu kauli za baadhi ya mikondo inayodai kuwa misimamo hii inaiweka Lebanon katika hali isiyotakiwa, alisema: Wale wanaoiuza Lebanon kwa utawala wa Marekani na kutekeleza mradi wa Kimarekani–Kizayuni, hao ndio waliolifikisha taifa katika hali hii.

Akirejea nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alisisitiza: Pigo kubwa zaidi kwa Marekani na utawala wa Kizayuni lilikuwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuanzishwa kwa Jamhuri ya Kiislamu. Iran imeendelea kubaki mfano wa uhuru na kujitegemea, na imefanikiwa kupiga hatua katika nyanja za kielimu, kijamii, kimaadili na kitamaduni, na kutoa kielelezo cha mafanikio ya nchi huru.

Katibu Mkuu wa Hezbollah, akirejea msimamo wa Iran dhidi ya mashambulizi ya hivi karibuni, aliongeza kusema: Iran ilikabiliana na siku 12 za vita na uvamizi, na kwa umoja na mshikamano wa wananchi sambamba na uongozi, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi (IRGC) na vyombo vya usalama, iliweza kuzima mipango ya Marekani na utawala wa Kizayuni.

Sheikh Naim Qassem, akisema kuwa visingizio vya Marekani vimepitwa na wakati, alisema: Lengo la kweli la Marekani ni ukoloni na kuitawala dunia, si Iran pekee. Katika kipindi cha hivi karibuni, walijaribu kuitikisa Iran kutoka ndani kwa kutumia vibaya matatizo ya kiuchumi na kijamii, na kwa kupenyeza waharibifu kwenye maandamano halali ya wananchi, wakatekeleza mauaji, uharibifu na uchomaji wa mali za raia.

Akirejea maendeleo ya eneo, alisisitiza: Mauaji ya halaiki kwenye Ukanda wa Ghaza ni dhihirisho la ukatili na uhalifu wa wazi, na yanaonesha ushiriki wa moja kwa moja wa Marekani na nchi za Magharibi. Pia, uvamizi wa Kimarekani–Kizayuni dhidi ya Lebanon hauwezi kuhalalishwa kwa madai ya kuogopa nia za muqawama, kwa kuwa adui yuko waziwazi katika uvamizi.

Kwatika khutuba yake Katibu Mkuu wa Hezbollah, huku akisisitiza mantiki ya muqawama alisema: Simulizi la ubeberu wa kimataifa—Marekani, utawala wa Kizayuni na washirika wao—linajengwa juu ya kusalimu amri mbele ya madhalimu; na kile kinachoitwa “amani kwa nguvu” kwa hakika ni ukoloni na udikteta kwa nguvu. Kusalimu amri kunamaanisha kupoteza kila kitu bila kikomo, lakini kujilinda hufungua mlango wa uwezekano na fursa nyingi.

Aliongeza kusema: Msitutie hofu kwa kifo; kifo hakiko mikononi mwenu, kiko mikononi mwa Mungu. Lakini heshima na utu viko mikononi mwetu, na hatutaviacha, kwa kuwa huu ni wajibu wetu.

Sheikh Qassem, akitahadharisha kuhusu athari za vita vyovyote dhidi ya Iran, alisema: Vita vyovyote dhidi ya Iran vinaweza kuliwasha eneo zima. Iran kwa miaka 43 imekuwa ikiunga mkono miqawama, na imeendeleza uungaji mkono huo ndani ya uhalali wa ukombozi wa ardhi, ilhali Marekani, utawala wa Kizayuni na washirika wao, kwa kuidhoofisha Lebanon na kuchochea migawanyiko, kivitendo wanaiunga mkono Israel.

Alisisitiza kuwa: Iran ina haki ya kumiliki teknolojia ya nyuklia ya amani, nguvu ya makombora na zana nyingine za ulinzi, kuwaunga mkono waliodhulumiwa na kuwa na jamhuri huru; lakini Marekani inapinga haki hizi, na hata zaidi ya hapo, inalenga kuiangamiza mifano hii.

Mwisho, Katibu Mkuu wa Hezbollah, akituma salamu na heshima kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, aliwaambia wananchi wa Iran: “Ninyi ni jiwe la thamani la taji. Sisi tuko pamoja nanyi, na ninyi mko pamoja nasi.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha