Ijumaa 30 Januari 2026 - 00:00
Viongozi wa dini wa Lebanon wawaunga mkono wananchi na Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Hawza/ Kikao cha mshikamano na maelewano kati viongozi wa dini wa Lebanon kilichokuwa na kaulimbiu isemayo “Taifa la Iran litavunja fitina na waanzilishi wake na kuzima malengo ya uvamizi” kilifanyika, ambapo washiriki walitangaza kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya mashambulizi na njama mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kikao hicho kilifanyika mjini Beirut kwa ushiriki na uratibu wa vyama, makundi na watu mashuhuri wa kitaifa wa Lebanon, pamoja na Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu na mkusanyiko wa Watu Huru kwa Ajili ya Lebanon, kwa lengo la kutangaza mshikamano na maelewano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika kikao hicho, ambacho kilihudhuriwa na Sayyid Mohammad Reza Mortazavi, mshauri wa masuala ya kitamaduni, pamoja na Tawfiq Samadi, kaimu balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon, washiriki kutoka jumuiya zote, makabila yote na madhehebu yote ya Lebanon walitangaza uungaji mkono wao thabiti na usio na masharti kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mapinduzi ya Kiislamu, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, pamoja na taifa la Iran lenye kusimama kidete na kishujaa, dhidi ya mashambulizi na njama.

Walisisitiza kuwa; ushiriki huu mpana unaashiria umoja na mshikamano wa nguvu za kitaifa, Kiislamu, Wakristo na Madruzi wa Lebanon katika kukabiliana na miradi ya fitina na uvamizi inayoilenga Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mkutano huu, zaidi ya kuwa ni msimamo wa ishara tu, unaonesha uhusiano wa kina kati ya mhimili wa Muqawama na nguvu za kisiasa, kidini na za wananchi nchini Lebanon na Palestina, ambao wanaiona Iran si tu kama mhusika wa kikanda, bali kama nguzo kuu ya uhuru, muqawama na kuyaunga mkono mataifa yaliyodhulumiwa.

Ujumbe mkuu wa kikao hiki ulikuwa ni miradi ya fitina, kuyumbisha utulivu na mashinikizo ya nje dhidi ya Iran, mbele ya umoja wa ndani, uongozi wenye hekima na uungaji mkono wa wananchi na wa kikanda.

Tawfiq Samadi, kaimu balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon, alisema kuwa; maendeleo ya hivi karibuni katika hatua mbalimbali za mgogoro yamefichua wazi tabia ya kihalifu ya wahusika wa nje, hasa kupitia kuchochea baadhi ya mamluki wa ndani kutekeleza vitendo vya hujuma.

Aliendelea kusema: Aidha, miongozo na maagizo ya nje kutoka kwa serikali ya Trump na Netanyahu, pamoja na maungamo ya wachochezi wa ghasia, yote yamesababisha kufichuka kwa uwazi vipengele vya njama iliyokuwa imeilenga Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hata hivyo, Iran, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, maelekezo ya hekima ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na juhudi pamoja na msimamo thabiti wa taifa shujaa la Iran, iliokoka salama kutokana na njama hiyo.

Baada ya hapo, Rabi‘ Bannat (Ahlus-Sunna), rais wa Jumuiya ya Kisoshalisti ya Kijamii, alisema katika hotuba yake kuwa kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran si kwa misingi ya heshima za juu juu au maslahi ya muda, bali kuunatokana na uaminifu; kwa sababu Iran imekuwa daima pamoja nasi na haijawahi kutuacha katika hali yoyote ile.

Sheikh Ghazi Hanina (Ahlus-Sunna), mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu mjini Beirut, huku akisisitiza nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alisema kuwa Iran ni nchi iliyochora sera zake kwa kaulimbiu ya ubinadamu na kuwatetea waliodhulumiwa, na daima imekuwa msaidizi wa wanyonge duniani.

Aliongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetetea heshima ya mwanadamu duniani kote, Syria, Yemen, Lebanon na Palestina ni mifano halisi ya ukweli huu. Hivyo basi, ni wajibu wetu kumuunga mkono kikamilifu Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi na uongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na sera za uhasama na uvamizi za serikali ya Marekani, hususan ya Donald Trump.

Iran ni alama ya heshima, utu, uhuru na kushikamana na msimamo wa Imam (r.a.) na uongozi

Rafi Madayan (Mkristo), katibu mkuu wa Mkutano wa Watu Huru kwa Ajili ya Lebanon, alisema kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamekuwa injini ya kuamsha mienendo ya kibinadamu katika eneo; mienendo inayopanda mbegu za wema, ukombozi na uhuru wa mataifa mbele ya madhalimu wa kishetani wanaoongozwa na Marekani.

Aliongeza kuwa; Iran leo inaendesha mapambano ya uhuru wa maamuzi na matakwa ya kitaifa yake dhidi ya watawala na watawala wa kimabavu wanaoongozwa na Marekani.

Sheikh Zuhair Ju‘ayd (Ahlus-Sunna), katibu mkuu wa Jabhat al-‘Amal al-Islami, alisema: Iran, ahadi na agano lake ni agano la muqawama na umoja wa Kiislamu, na kwa sababu hiyo tumesimama pamoja na Iran na tunaendelea kuiunga mkono. Iran ni alama ya heshima, utu, uhuru na kushikamana na msimamo wa Imam Khomeini (r.a.), na leo pia, kama mapinduzi ya wanyonge, chini ya uongozi wa Ayatullah Imam Khamenei (Mola aendelee kumuhifadhi), inaendelea na njia yake.

Shakir Barjawi (Ahlus-Sunna), kiongozi wa Harakati ya Tauhidi ya Kiarabu, alisisitiza: Tunatangaza mshikamano wetu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa sababu bendera hii ni bendera iliyoinuliwa kutoka mbinguni mwa Hussein (a.s.), na imehamasishwa na wito wa milele wa “Hayhat minna adh-dhillah” (uwe mbali nasiudhalili).

Mahmoud Qamati (Mshia), waziri wa zamani na makamu wa rais wa Baraza la Kisiasa la Hezbollah, alisema kuwa; Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mfano wa haki, mapinduzi, uhuru, uadilifu, ushindi na uhuru wa kweli. Iran si ya Mashariki wala ya Magharibi, bali imewasilisha duniani mfano wa ustaarabu wa Kiislamu; mfano uliong’ara katika nyanja za elimu, anga za juu, huduma kwa wananchi, usalama, nguvu na kukabiliana na dhulma ya kimataifa ya Marekani — ambayo leo imejidhihirisha katika sura ya Trump.

Aliongeza kusema: Tumesimama pamoja na Iran; Iran ambayo imekuwa ikiunga mkono na inaendelea kuunga mkono muqawama wetu. Tumesimama pamoja na Waliyyul-Faqih, Ayatullah Imam Khamenei (Mola amuhifadhi), kiongozi ambaye ametusaidia katika ukombozi wa ardhi yetu na bado yuko pamoja nasi, ili tuishi kwa heshima na fahari, na tushinde juu ya maadui wa Umma wetu, yaani Wazayuni na Wamarekani.

Ralph Shamali (Mkristo), rais wa Humat ad-Diyar – Walinzi wa Ardhi, alimuelezea adui mkuu kuwa ni utawala wa Kizayuni, na akaongeza: Tunaishukuru Iran kwa kutuunga mkono sisi na muqawama wetu, na kwa kutuweka bega kwa bega na Hezbullah katika kukabiliana na utawala haram wa Kizayuni, kwa heshima na taadhima.

Suhail (Suhayb) Sha‘ban (Ahlus-Sunna), mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Tauhidi ya Kiislamu, aliisifu hekima na umakini wa taifa la Iran katika kukabiliana na fitina, na kusema: Taifa la Iran, kwa hekima na mtazamo wake wa kina, liliweza kuizima fitina iliyopangwa dhidi yake katika muktadha wa vita vikali na vya pande zote zilivyoandaliwa na Marekani kwa ushirikiano wa utawala wa Kizayuni na pia nchi za Ulaya.

Sheikh Abdullah Jabri (Ahlus-Sunna), rais wa Harakati ya Umma, alisema kuwa ni lazima tuwe macho kuhusu mradi unaopangwa wa kuzigawanya nchi za eneo. Ikiwa hatutatekeleza wajibu wetu wa kihistoria ipasavyo, tutashindwa; lakini kwa uelewa, busara, hekima na kadhalika, tutaizima fitina ya maadui na kuifelisha mipango yao.

Mahfouz al-Munawwar (Ahlus-Sunna), mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina, alisema: Iran ilibadilika kutoka nchi iliyokuwa ikiunga mkono utawala wa Kizayuni na kuwa nchi inayounga mkono Palestina. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa pamoja na taifa la Palestina lililodhulumiwa na imekuwa ikiliunga mkono.

Alisisitiza: Tangu wakati ambao Imam Khomeini (r.a.) alipokuwa uhamishoni, alikuwa akiunga mkono suala la Palestina na alitoa kaulimbiu ya “Leo Iran, kesho Palestina.” Huu ndio mkondo ambao kiongozi wetu, Ayatullah Imam Khamenei (Mola amuhifadhi), ameendelea kuufuata kwa uthabiti kwa zaidi ya miongo mitatu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha