Alhamisi 29 Januari 2026 - 23:00
Uongozi wa hekima wa Ayatollah Khamenei unahakikisha mwendelezo wa ushindi

Hawza/ Ayatollah Sayyid Yasin Mousawi, katika tamko lake, ameutaja uongozi wa hekima wa Mtukufu Ayatollah Khamenei kuwa ni ufunguo wa kuendelea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu—ikiwemo ushindi wa hivi karibuni dhidi ya njama za adui—na amesisitiza kuwa njia hii itaendelea hadi bendera itakapokabidhiwa kwa mwenyewe halisi.

Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Sayyid Yasin Mousawi, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Baghdad, katika tamko lake huku akirejelea njama za hivi karibuni za maadui ambazo kilele chake kilijidhihirisha katika machafuko ya siku za tarehe 18 na 19 ya mwezi wa Dey, alisisitiza kushindwa kabisa kwa njama hizo. Alitaja maandamano makubwa ya wananchi yaliyofanyika tarehe 12 January yaliyokuwa na lengo la kuunga mkono mfumo wa Kiislamu kuwa ni jibu thabiti na hatua ya kihistoria ambayo, kwa uongozi wa Kiongozi wa Mapinduzi, yalibadilisha njama hiyo kuwa ushindi mpya kwa Mapinduzi ya Kiislamu na ushindi wa matakwa ya wananchi dhidi ya miradi ya ubeberu duniani.

Matini kamili ya tamko la khatibu wa Ijumaa wa Baghdad ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:


“Na wakitaka kukusaliti, basi kwa hakika walimsaliti Mwenyezi Mungu hapo kabla, naye akakupa uwezo juu yao; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.”
(Sura al-Anfal, Aya ya 71)

Tunalitangazia taifa shujaa na lenye kusimama imara la Iran, na mataifa yote yaliyodhulumiwa duniani, kwamba yale yaliyofanywa na vibaraka wa ukoloni wa Marekani na Israel—kwa kumsaliti Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mtume wake na Maimamu watoharifu (amani iwe juu yao)—ikiwemo uharibifu, uvamizi na mauaji ya idadi ya vijana wetu, wawe ni majeshi ya usalama, raia au wasio na hatia; pamoja na kuchomwa moto misikiti, husseiniyya, maeneo matukufu ya kuzuru na vitendo vingine vya kihalifu—yote yalifanyika katika muktadha wa juhudi za maadui kwa lengo la kuuangusha Uislamu na Jamhuri yake tukufu nchini Iran, ardhi ya itikadi na shahada. Hata hivyo, njama zote hizo zilipotea bure, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akaisaidia dini na dola yake.

Kama ambavyo Mapinduzi haya yenye baraka, katika kipindi cha karibu nusu karne, yamewashinda Wamarekani na vibaraka wao katika njama zote na kurejesha hila zao juu yao wenyewe; na kama alivyosema mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu, Imamu Khomeini (Mwenyezi Mungu aitukuze siri yake), baada ya kuuawa shahidi Ayatollah Beheshti: “Msihangaike… bendera yetu haitaanguka mpaka mwenyewe aipokee”—na alimaanisha Imamu Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake)—safari hii pia nusra ya Mwenyezi Mungu ilipatikana.

Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mara nyingine aliisaidia dini na dola yake dhidi ya wapanga njama, wasaliti na wakoloni, katika siku mpya na adhimu miongoni mwa Siku za Mwenyezi Mungu; siku ambayo Imamu Khamenei aliitaja kama siku ya kihistoria na ya fahari ya 12 Januarya. Baada ya siku ya “22 Bahman” kuwa siku ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuasisiwa kwa Jamhuri, siku ya “12 January” ikawa siku ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kuwazuia maadui; siku ya kudumu Mapinduzi ya Kiislamu na dola yake:


“Nao wanapanga hila, na Mwenyezi Mungu anapanga hila; na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa wapangaji.”
(Sura al-Anfal, Aya ya 30)

Ushindi huu ambao taifa la Iran limeupata ni ushindi kwa Uislamu na kwa mataifa yote ya Kiislamu, hususan Mashia wa Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao) Mashariki na Magharibi ya dunia. Ushindi huu utaendelea kwa hekima na uongozi wa sayyid na kiongozi wa Umma, Ayatollah Imamu Khamenei, hadi utakapokabidhiwa kwa mwenyewe Imamu wa Zama (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake).

28 Rajab al-Khayr 1447 Hijria Qamaria
Najaf Ashraf / Kando ya Haram ya Amirul-Mu’minin (amani iwe juu yake)

Yasin Mousawi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha