Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Abu Alaa’ al-Walai, Katibu Mkuu wa Kata’ib Sayyid al-Shuhadaa ya Iraq, katika kauli zilizonukuliwa na vyombo vya habari vilivyo karibu na mkondo wa muqawama, alisisitiza kile alichokiita “muunganiko wa kiitikadi na kisiasa wa makundi ya muqawama na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran”, na akasema kuwa msaada wa Mwenyezi Mungu kwa nchi hiyo ni “wa hakika na wa kudumu”.
Akiashiria simulizi ya kihistoria, alitoa mtazamo kwamba “ushindi daima huwa upande wa muqawama wenye heshima”, na akaelezea matukio ya sasa kuwa ni muendelezo wa misingi na desturi za kihistoria.
Al-Walai, katika sehemu ya hotuba yake akimuelezea Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alizungumza kuhusu ushirikiano kamili wa harakati hili pamoja naye, na akautaja msimamo huo kuwa ni dalili ya “kujizatiti kwa vitendo Jumuia ya muqawama chini ya uongozi wa kidini na kisiasa”.
Katibu Mkuu wa Kata’ib Sayyid al-Shuhadaa ya Iraq pia, akieleza vigezo vya uongozi kwa mtazamo wa mkondo huu, alitaja sifa kama imani, ujasiri, ukweli, ikhlasi na ufaqihi kuwa ni misingi ya uhalali wa uongozi.
Aliendelea kwa kukosoa vikali sera za Marekani, na akaishutumu Ikulu ya White House kwa “kuvunja ahadi na kutenda uhalifu”. Al-Walai alisema kuwa Marekani, kwa kuyakalia mataifa na kuweka shinikizo kwa watu, imesababisha kuyumba kwa uthabiti wa eneo hili.
Mwisho, alisema kwamba mkondo wa muqawama kuikabili Marekani ni sawa na imani kumkabili tw'aghuti”, na akadai kwamba katika makabiliano hayo, Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni “kielelezo cha imani”, huku rais wa Marekani akiwa ni “kielelezo cha tw'aghuti”.
Maoni yako