Alhamisi 18 Desemba 2025 - 22:40
Adui Mzayuni Hawezi Kujisalimisha na Kuachia Nafasi Katika Ukanda Huu

Hawza/ Sheikh Ali al-Khatib, Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia wa Lebanon, alisisitiza: Tunaupa umuhimu uthabiti katika nchi zote za eneo hili, lakini adui Mzayuni haachi nafasi yoyote kwenye uthabiti huo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ali al-Khatib, Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia wa Lebanon, katika kikao chake na Karolina Lindholm Billing, mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Wakimbizi nchini Lebanon, kilichofanyika katika makao makuu ya Baraza la Kiislamu la Mashia katika eneo la Hazmieh, alisisitiza kuwa: Tunaupa umuhimu uthabiti katika nchi zote za eneo hili, lakini adui Mzayuni haachi nafasi yoyote katika uthabiti huo, na hata haheshimu mashirika yanayohusiana na Umoja wa Mataifa wala sheria za kibinadamu za kimataifa.

Sheikh al-Khatib, akieleza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akiwaza kuhusu sehemu ya wakimbizi wa Syria waliokuja Lebanon baada ya kuanguka kwa serikali ya awali ya Syria, kwa sababu hawakutendewa kama wale waliokuja hapo awali, alisema: Nimefurahi kusikia kutoka kwenu kwamba mko tayari kusaidia kundi hili. Sisi tunaunga mkono kurejea kwa wakimbizi wote katika ardhi na nchi zao, na suala hili ni mzigo mzito kwa Lebanon kwa nyanja za kiuchumi, kijamii na kiusalama.

Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Mashia aliongeza: Tumejitolea kwa sheria za kimataifa na taasisi za kibinadamu, hasa Kamishna Mkuu wa Wakimbizi; taasisi ambayo ina nafasi muhimu sana ya kibinadamu, na sisi daima tunaunga mkono jukumu hili kwa upande wa kimaadili.

Alisema: Chanzo cha ukimbizi ni cha kisiasa, na kwa kiasi kikubwa kina mizizi ya Wazayuni; kwa sababu utawala wa Israel una jukumu la msingi katika kuchezea ramani za eneo na matokeo yake yasiyo na uthabiti.

Sheikh al-Khatib aliendelea: Kwa bahati nzuri, leo kuna mabadiliko katika uelewa wa maoni ya umma wa dunia kuhusu nafasi halisi ya utawala wa Kizayuni, na jambo hili linaimarisha msimamo wa Kamisheni, na ninyi kwa hakika ni mashahidi wa mashambulizi haya; iwe ni Gaza au kusini mwa Lebanon.

Akisisitiza kwamba tuko tayari kwa aina yoyote ya ushirikiano utakaorahisisha dhamira yenu, na tuna hamu ya kufahamu kiwango cha msaada wenu kwa wakimbizi wa Syria walioingia Lebanon baada ya kuanguka kwa serikali ya awali ya Syria, alisema: Tunashukuru kila jitihada inayofanywa na Kamishna wa Wakimbizi kuwasaidia wakimbizi hawa, na tunatumaini wigo wa msaada wa Kamisheni utajumuisha pia wakimbizi wa Lebanon waliotokana na mashambulizi ya Israel.

Kauli za Karolina Lindholm Billing

Katika kikao hiki, Billing alisema: Takribani miezi miwili sasa nimewasili Lebanon, nimekutana na viongozi wote, na nina hamu ya kukutana pia na viongozi wa kidini. Ninajivunia kuanza mikutano hii pamoja nanyi.

Akiainisha kuwa jukumu la Kamisheni ni kuisaidia Lebanon katika hali ya dharura, na kwamba jamii ya Mashia imepata madhara na shinikizo kubwa katika vita vya hivi karibuni, alisema: Tuna wajibu pia kuhusu wakimbizi wa Syria, na baada ya kuanguka kwa serikali ya Syria jukumu hili limekuwa hai zaidi.

Billing alisema: Tunataka kusikia maoni yenu kuhusu namna ya kuimarisha shughuli hizi kwa wakimbizi walioingia Lebanon baada ya kuanguka kwa serikali ya Syria. Tunashirikiana kwa karibu katika suala hili na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Umma, Brigedia Jenerali Hasan Shaqir, pamoja na magavana.

Akielezea kuwa jukumu letu ni la kibinadamu na tunajitahidi kuwasilisha taswira halisi ya matukio nchini Lebanon na mwenendo wa Israel kwa jumuiya ya kimataifa, alisema: Tunajua kuwa Lebanon, ikilinganishwa na idadi ya watu wake, imebeba mzigo mkubwa zaidi wa kupokea wakimbizi; kwa hivyo tumeiomba serikali ya Lebanon iwasajili wakimbizi wapya wa Syria ili tuweze kubaini aina na kiwango cha wakimbizi wa kimataifa wa kuwasaidia.

Mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliendelea kueleza kuwa; katika kikao chetu cha hivi karibuni na Tareq Mitri, Naibu Waziri Mkuu wa Lebanon, tuliwasilisha ombi hili, hasa kwa kuwa wakimbizi wapya hawajatendewa kama makundi ya awali.

Aliongeza: Tumetoa misaada kwao, na katika siku za karibu tutatembelea maeneo ya Biqaa na kaskazini ili kuchunguza hali zao kwa usahihi zaidi; kwa hivyo ni muhimu kuanzisha uratibu rasmi zaidi kati ya Kamisheni na serikali kwa lengo hili.

Billing alisisitiza: Kurejea nyumbani bado ni kanuni ya msingi, na hadi sasa karibu mafaili laki 4 yamefungwa; jitihada zitaendelea mwaka ujao pia ili kuharakisha kufungwa mafaili haya na kuwarejesha katika ardhi yao, ili wasirejee Lebanon.

Pia alisema: Katika kipindi cha vita vya hivi karibuni vya utawala wa Kizayuni, Kamisheni pia ilichukua nafasi katika kutoa misaada kwa wakimbizi wa Lebanon, na ikawasaidia katika maeneo ya kusini kwa njia mbalimbali, iwe moja kwa moja au kupitia taasisi kama Msalaba Mwekundu, Ulinzi wa Raia na Usalama wa Umma; pia baadhi ya familia zenye mahitaji zilipata msaada wa kifedha moja kwa moja.

Kikao na ujumbe wa Maaskofu wa Antonia

Sheikh Ali al-Khatib pia alikutana na ujumbe wa maaskofu wa Antonia ukiongozwa na Askofu Boutros Azar na Askofu Beshara Elia. Katika kikao hiki, masuala ya jumla ya nchi yalijadiliwa.

Sheikh al-Khatib alisisitiza katika kikao hicho: Umuhimu wa umoja wa kitaifa katika kukabiliana na awamu ngumu ambayo nchi yetu inakabiliwa nayo chini ya mashambulizi ya Israel unahisiwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Mwisho, Askofu Elia alimkabidhi Sheikh Ali al-Khatib vitabu vyake viwili vyenye majina: “Hati ya Udugu wa Kibanadamu: Usomaji wa Kitaaluma” na “Usomaji wa Kitaaluma kutoka katika Nyaraka za Kinabii hadi Hati ya Udugu wa Kibanadamu.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha