Jumamosi 6 Desemba 2025 - 23:10
Sheikh Jalala Afanya Ziara ya Kushtukiza Katika Markaz ya Imam Ridhwa (a.s) Arusha Tanzania + Picha

Hawza/ Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, ameendelea na ziara zake mkoani Arusha ambapo leo tareh 6 December amefanya ziara ya kushtukiza katika Markaz (Husainia) ya Imam Ridhwa (a.s), inayosimamiwa na taasisi ya Sayyid Shuhadaa Arusha.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika ziara hiyo iliyokuwa na lengo la kuimarisha mafungamano na uhusiano bora miongoni mwa Waislamu wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbayt (as), Sheikh Jalala alipata fursa ya kutembelea Markaz hiyo iliyopo chini ya usimamizi wa Sheikh Maulid Hussen Sombi, huku lengo kuu la ziara likiwa ni kuimarisha mahusiano ya kitaasisi pamoja na kuhuisha umoja na mshikamano miongoni mwa Mashia kama tulivyo ashiria hapo awali.

Aidha, Sheikh Jalala pia alitoa pongezi kwa taasisi ya Sayyid Shuhadaa kutokana na juhudi zake za kuendelea kueneza elimu ya dini, kukuza maadili mema na kutoa huduma mbalimbali za kijamii, vilevile alisisitiza umuhimu wa taasisi za Kiislamu kuendeleza ushirikiano, mawasiliano na mshikamano kwa ajili ya maslahi mapana ya umma na ustawi wa jamii.

Kwa upande wake, Sheikh Maulid Hussen Sombi aliushukuru uongozi wa Jumuiya ya Shia Ithnaasharia Tanzania (TIC) pamoja na taasisi ya Imam Swadiq (a.s) kwa jitihada zao za kuimarisha umoja wa Mashia, kufanya ziara zenye lengo la kuunganisha udugu na kudumisha mahusiano mema baina ya taasisi mbalimbali za kidini. Alieleza kuwa ziara hizo zina mchango mkubwa katika kuimarisha mshikamano na maendeleo ya shughuli za kidini.

Sheikh Jalala Afanya Ziara ya Kushtukiza Katika Markaz ya Imam Ridhwa (a.s) Arusha Tanzania + Picha

Sheikh Jalala Afanya Ziara ya Kushtukiza Katika Markaz ya Imam Ridhwa (a.s) Arusha Tanzania + Picha

Sheikh Jalala Afanya Ziara ya Kushtukiza Katika Markaz ya Imam Ridhwa (a.s) Arusha Tanzania + Picha

Sheikh Jalala Afanya Ziara ya Kushtukiza Katika Markaz ya Imam Ridhwa (a.s) Arusha Tanzania + Picha

Sheikh Jalala Afanya Ziara ya Kushtukiza Katika Markaz ya Imam Ridhwa (a.s) Arusha Tanzania + Picha

Mishoni ziara hiyo ilihitimishwa kwa dua maalumu iliyolenga kumuomba Mola adumishe umoja, mshikamano na maendeleo kwa Waislamu wote Ulimwenguni.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha