Alhamisi 18 Desemba 2025 - 19:40
Kikao Kilicho na Anuani Isemayo: “Sitisheni Mauaji ya Kimbari Dhidi ya Wapalestina” Chafanyika Nchini India

Hawza/ Kikao chenye anuani isemayi “Sitisheni mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina, ikomboleni Palestina” kilifanyika katika mji wa Hyderabad, India, kwa lengo la kutangaza mshikamano na taifa lililodhulumiwa la Palestina na kulaani vikali uhalifu wa utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika kuendeleza juhudi za kuonesha mshikamano na taifa la Palestina linalodhulumiwa, pamoja na kulaani uhalifu na uvamizi unaoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni, kikao hicho kilifanyika mjini Hyderabad.

Lengo kuu la mkutano huu lilitangazwa kuwa ni kuchambua maendeleo ya hivi karibuni yanayohusiana na suala la Palestina, kufafanua vipengele mbalimbali vya uhalifu wa utawala wa Kizayuni, pamoja na kuimarisha mshikamano wa wananchi na wa kimataifa na taifa la Palestina.

Hujjatul-Islam Sayyid Taqi Reza Abedi, kiongozi wa kidini wa Kihindi na mjumbe wa Kamati ya Hija, katika kikao hiki alieleza kwa kina dhulma inayowakabili wananchi wa Palestina na kusisitiza wajibu wa kibinadamu, kimaadili na kidini katika kutetea haki halali za taifa hili.

Miongoni mwa mambo yaliyojitokeza kwa uwazi katika mkutano huu ni ushiriki mkubwa na wenye athari wa watu mashuhuri wasiokuwa Waislamu katika kuunga mkono taifa la Palestina; jambo linaloonesha asili ya ubinadamu na ya kuvuka mipaka ya dini ya suala la Palestina, pamoja na upana wa uungaji mkono wa wananchi kwa taifa hili lililodhulumiwa katika ngazi mbalimbali za kijamii na kifikra.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha