Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Pedro Sánchez katika hotuba yake alieleza kwamba Uhispania, baada ya kuanza kwa vita vya kikatili na mauaji ya kimbari ya Israel huko Ghaza, ilichukua hatua ya kuitambua nchi ya Palestina mapema kuliko wengine. Wakati huo, uamuzi huu wetu ulikumbana na upinzani mkali wa wapinzani wa kisiasa na shinikizo la kidiplomasia kutoka kwa washirika.
Alisisitiza kwamba licha ya hayo, mwaka mmoja baadaye, nchi nyingine zimechukua hatua zinazofanana kwa kufuata nyayo zetu, jambo linaloashiria mabadiliko mapana zaidi katika mtazamo wa kimataifa. Alisema: “Muda umetuthibitishia kwamba tulikuwa sahihi.”
Waziri Mkuu wa Uhispania pia alitaja hatua mahsusi zilizochukuliwa na serikali yake, miongoni mwao ikiwa ni kusitisha kabisa usafirishaji wa silaha kwenda Israel na kuongeza misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina.
Aliyataja hatua hizi kuwa ni sehemu ya sera ya nje iliyo thabiti, yenye mizizi katika mfumo wa pande nyingi, uthabiti na mshikamano wa kimaadili, na akasisitiza kwamba Uhispania haiwezi kubaki upande wowote mbele ya vifo vingi vya raia na watoto pamoja na uharibifu wa jamii nzima ya kibinadamu.
Chanzo: SAFA NEWS
Maoni yako