Ijumaa 9 Mei 2025 - 00:10
Athari kubwa za Hawza ya Qum zimeenea duniani kote

Katibu Mkuu wa Hizbullah Lebanon ameeleza athari na baraka za Hawza ya Qum zimeenea katika uwanja wa kitamaduni na kijamii, hasa katika suala la kuunda Mapinduzi ya Kiislamu na mhimili wa muqawama.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika ujumbe wa Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Na’im Qasim, Katibu Mkuu wa Hizbullah Lebanon, kwenye Kamisheni Maalumu ya Hawza katika kongamano la kimataifa la miaka mia moja tangia kuanzishwa upya Hawza ya Qum, ujumbe ambao uliosomwa leo asubuhi katika shule ya Imam Kadhim (a.s) mjini Qum, imetajwa kuwa: Mtume Mtukufu (s.a.w.w) amewataja watu wa elimu na jihadi kuwa ndio watu wa karibu kabisa na Mitume. Imam Ali (a.s) naye amesema kuwa, maulamaa wanabaki katika fikra na kumbukumbu za watu kwa sababu ya elimu yao, hata kama hawatokuwepo tena miongoni mwa watu.

Hawza ya Qum imekuwa na athari kubwa katika kueneza dini halisi ya Muhammadiyya (s.a.w.w) ndani ya Iran na katika nchi zote zilizoathiriwa nayo.

Kuanzishwa kwa Hawza hii kumeleta athari za kina katika nyanja za falsafa, utamaduni na jamii. Athari hizi zimesambaa kutoka Qum hadi katika nchi nyingine pia.

Moja ya athari muhimu zaidi za Hawza ya Qum ni kuhuisha Hadithi na Fiqhi ya Ahlul Bayt (a.s), jambo ambalo kwa mtazamo thabiti, limeweza kuhuisha maarifa haya katika nyanja mbalimbali.

Miongoni mwa athari muhimu za Hawza ya Qum na Mapinduzi ya Kiislamu ni mhimili wa muqawama, ambao umesimama kidete dhidi ya upanuzi wa Israel na madhalimu wakubwa duniani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha