Jumatano 17 Desemba 2025 - 18:00
Tuwe Wapinga-Uzayuni, si Wapinga-Uyahudi

Hawza/ Harakati ya kuunga mkono Palestina nchini Scotland ililaani tukio la ufyatuaji risasi uliosababisha vifo katika hafla ya Wayahudi nchini Australia, na ikasisitiza kuwa hakuna uhalali wowote wa kuwaua watu kwa misingi ya dini, rangi au utaifa. Harakati hiyo ikaonya kuwa tukio hili halipaswi kuondoa mwelekeo wa kuzingatia mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, shirika la “Scottish Palestine Solidarity Campaign” katika tamko lake rasmi lililaani kutokea kwa tukio la ufyatuaji risasi uliosababisha vifo katika moja ya hafla za Wayahudi nchini Australia. Taasisi hii ya kiraia ilisisitiza kuwa hakuna uhalali wowote wa kuua watu kwa sababu tu ya utaifa, rangi, kabila au dini yao.

Katika tamko rasmi la harakati hiyo imeelezwa kuwa; Wayahudi kwa ujumla hawawajibiki katika mauaji ya kimbari yanayofanywa na Waisraeli, kama ambavyo si Waislamu wote wanaowajibika kwenye vitendo vya makundi ya kigaidi, wala si raia wote wa Marekani wanaowajibika kwenye sera za Donald Trump.

Harakati hiyo imeonya kuwa; haitaruhusu janga hili lililotokea Australia kugeuza mwelekeo wa kupinga mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina, ambayo kwa mujibu wao yanaungwa mkono na baadhi ya wanasiasa wa Magharibi.

Tamko hilo pia limesisitiza kuwa; mahakama za Scotland kwa muda mrefu zimekuwa zikitofautisha kati ya chuki dhidi ya Wayahudi na upinzani dhidi ya Uzayuni, na zimeutaja ufyatuaji risasi wa leo kuwa ni mfano wa chuki dhidi ya Uyahudi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha