Jumanne 6 Mei 2025 - 12:57
Hawza ndio taasisi pekee inayojenga ustaarabu na kumjenga mwanadamu duniani

Suheil As'ad alisisitiza kuwa: Hawza, hasa Hawza ya Qum, ndio taasisi ya kidini duniani ambayo imeweza kuchukua nafasi muhimu katika mchakato wa kujenga ustaarabu mpya wa Kiislamu na kulea watu wenye athari katika nyanja za muqawama, siasa na utamaduni.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, kutoka Mashhad, hawza katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran historia yake imejikita kwenye kuleta ustaarabu wa Kishia, na tangu zamani imekuwa ikichukua nafasi muhimu katika kuunda utambulisho wa kidini, kitamaduni na kisiasa kwenye jamii ya Kiislamu. Taasisi hii ya kielimu na kidini si tu imekuwa ikitayarisha wanazuoni waumini na wasomi wenye athari ndani ya nchi, bali pia imekuwa na uwepo wenye nguvu na wa kimkakati katika nyanja za kimataifa.

Kwa msingi huo, mwandishi wa shirika la habari la Hawza mjini Mashhad, kwa kuashiria historia na uwezo wa ustaarabu wa hawza, katika mahojiano maalumu na Suheil As'ad, mhubiri wa kimataifa mzaliwa wa Argentina na miongoni mwa wahitimu wa Hawza ya Qum, amezungumzia nafasi ya taasisi hii ya kielimu katika ujenzi wa ustaarabu mpya wa Kiislamu, uongozi wa kisiasa kwa jamii ya Kishia na athari zake katika uwanja wa kimataifa. Hii hapa ni sehemu ya mazungumzo hayo:

As'ad alitaja Hawza ya Qum kuwa ni kituo cha kielimu cha Kishia na miongoni mwa vyanzo muhimu katika kulea, kiakili na kiroho viongozi wa mrengo wa muqawama, na akasisitiza: Hawza ya Qum imekuwa na athari kubwa katika kuunda na kuelekeza nafsi na nyoyo za watu, hasa katika njia ya muqawama.

Akiendelea kueleza, alisema kuwa: Wahusika kama Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim Safiuddin ni miongoni mwa wale waliokuzwa katika mazingira ya kiakili na hawza, na akaeleza: Hawza, kama taasisi yoyote ya kielimu, inaweza kujenga sehemu tu ya shakhsia ya mwanadamu; lakini kile kinachomsawiri mtu kama Sayyid Hassan Nasrallah, ni kutumia kwa njia sahihi taasisi ya hawza, kuelewa kwa kina maarifa ya kidini, na kutekeleza kwa vitendo mafundisho ya dini katika maisha binafsi.

As'ad aliendelea kusema: Hawza pekee haijitoshelezi, bali kinacho mfanya mtu afikie katika ukamilifu, ni mwenendo, fikra, usomaji na juhudi binafsi zake binafsi.

Alisisitiza: Hawza peke yake haiwezi kuwa dhamana ya mafanikio ya kiroho na kiakili ya watu isipokuwa yule anayeitumia ajipange kwa maarifa, utendaji na ikhlasi.

"Kila tulichonacho kimetokana na hawza."

Mhubiri huyu wa dini katika uwanja wa kimataifa, akiashiria tajiriba yake binafsi ya kusoma Qum baada ya kuhama kutoka Argentina, alikiri: Kila nilichonacho leo kama mwanafunzi wa dini, mhubiri, sheikh na mwanaharakati wa kitamaduni, kina asili kutoka katika hawza ya Qum.

Aliashiria kwamba hawza pia, kama taasisi nyingine yoyote, ina mapungufu na kasoro, na akajiweka miongoni mwa wakosoaji wa hawza, kwa kusema: Ukosoaji wangu kuhusu hawza ni ukosoaji wa kimaendeleo, si wa kubomoa; na naiangalia hawza kama tunu yenye thamani ambayo inahitaji kupigwa msasa; kama dhahabu inayochimbwa kutoka mgodini ambayo inahitaji kusafishwa na kusukwa ili kufikia umbo lake la mwisho.

Hawza ni taasisi pekee kwa ajili ya kujenga ustaarabu na kumlea mwanadamu

As'ad, akiashiria uwezo wa kipekee wa hawza katika kuijenga jamii na ustaarabu wa Kiislamu, alisema: Hatuna chuo kikuu wala shule yoyote duniani inayoweza kulea shakhsia kama Imam Khomeini (r.a) au Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi (Ayatullah Khamenei). Kwa sababu ni hawza pekee yenye uwezo huo, na inapaswa kutumikiwa kwa namna ambayo wahitimu wake wote waweze kuwa watu wenye athari na wenye kujitolea katika kiwango cha kimataifa.

Matumizi bora ya uwezo wa hawza yanahitaji uelewa na upangaji Mhubiri huyu wa dini katika uwanja wa kimataifa alisisitiza: Matumizi sahihi ya hawza yanawezekana tu kwa kupitia upangaji mzuri, uelewa wa kina na mwenendo ulio sahihi, na iwapo hawza itatumika kwenye mtazamo huu, basi inaweza kulea wasomi na viongozi wenye ustaarabu mpya wa Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha