Jumamosi 10 Mei 2025 - 19:54
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa ataka hijabu ipigwe marufuku vyuoni

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Bruno Retailleau, jana alitangaza kuwa ana azma ya kuzuia uvaaji wa hijabu katika vyuo vikuu.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Waziri huyo jana katika kituo cha televisheni cha RMC nchini Ufaransa alisema kuwa anatamani uvaaji wa hijabu upigwe marufuku nchini Ufaransa.

Akasema: "Ninaamini kuwa hijabu si sehemu ya Uislamu wa asili na wa kitamaduni, bali ni imani ya kisiasa inayolazimishwa kwa wanawake, na ambayo inaweka mashaka juu ya usawa wa kijinsia."

Mnamo Machi 2004, serikali ya Ufaransa ilipitisha sheria ya kuzuia hijabu katika shule za msingi na sekondari, lakini haikuweza kutekeleza hilo vyuoni kutokana na msimamo thabiti na upinzani mkali wa wanafunzi Wakiislamu. Waziri wa sasa wa elimu Ufaransa ni Gabriel Attal, ambaye pia anaamini kuwa "vazi la hijabu ni vazi la kidini linalokiuka sheria za serikali ya raia."

Aidha, mnamo tarehe 18 Februari, Seneta ya Ufaransa ilipitisha muswada wenye lengo la kuzuia hijabu katika mashindano ya michezo nchini humo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha