Jumamosi 20 Desemba 2025 - 07:59
Lazima tuwe na uhuru wa kifikra na kielimu / Fikra za Magharibi Hazipaswi Kuathiri Jamii

Hawza/ Mtukufu Ayatullah Subhani alionya kwamba: Ni lazima tuingie katika uwanja wa elimu kupitia njia sahihi, wala hatupaswi kuvutiwa na kuathiriwa na Magharibi. Sisi wenyewe tuna misingi sahihi ya kifikra. Ni lazima tuwe na uhuru wa kifikra na kielimu, na fikra za Magharibi hazipaswi kuathiri jamii.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, hafla ya ufunguzi na kuanza rasmi kwa shughuli za Taasisi ya Utafiti wa Ilmu ya Kalamu ya Imam Ja‘far Sadiq (a.s) ilifanyika kabla katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Imam Ja‘far Sadiq (a.s) mjini Qum Iran. Katika hafla hiyo, Mtukufu Ayatullah Ja‘far Subhani, mmoja wa Maraji' wa Taqlidi, kwa kurejea asili ya pande mbili za mwanadamu, alifafanua mtazamo wa Uislamu kuhusiana na kuinuka kifikra na kimaadili.

Alieleza kwamba: Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Qur’ani Tukufu: “Na katika ardhi zipo ishara kwa wenye yakini; na ndani ya nafsi zenu (pia), je, hamtazami?” Mwanadamu ameumbwa kutokana na pande mbili: upande wa fikra na upande wa silika. Wanafalsafa wanaupa heshima upande wa fikra wa mwanadamu na humuita “mnyama mwenye mantiki”, na wanazuoni wa maadili pia hujikita katika upande wake wa kimaadili. Uislamu unazingatia pande zote mbili; upande wa kifikra na upande wa kimaadili.

Mtukufu Ayatullah Subhani aliendelea kwa kurejea aya za Qur’ani akasisitiza: Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani: “Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi na kupishana kwa usiku na mchana zimo ishara kwa wenye akili” na pia katika aya nyingine anasema: “Na kwa nafsi na kwa Yule aliyeiunda kwa uwiano; akaijuza uovu wake na ucha-Mungu wake.” Hivyo basi, ni madhehebu ya Kiislamu yaliyo kamili yanayozingatia pande zote mbili; yanakuza vipengele vya kifikra na pia kuiongoza silika kwenye njia sahihi.

Utafiti wenye athari; kigezo kikuu cha tafiti za kielimu za Hawza

Marjaa huyu wa Taqlidi, akirejea dhamira ya Taasisi mpya ya Utafiti wa elimu ya Kalamu ya Imam Ja‘far Sadiq (a.s), walibainisha: Kikao hiki kwa hakika kinahusiana na upande wa kwanza, yaani upande wa fikra na utafiti. Katika utafiti ni lazima kuzingatia daima kanuni hii kwamba mada ya utafiti ichaguliwe kwa namna itakayoweza kuwa na athari katika jamii na kuwa na manufaa kwake.

Akaongeza kusema: Ikiwa zipo mada ambazo hazichangii katika ukamilifu wa kifikra kwenye jamii au kwa sasa hazihitajiki, zinapaswa kuwekwa katika nafasi ya pili. Utafiti unapaswa kuwa na matunda, kiroho na kimada.

Umuhimu wa kuzingatia kwa pamoja sayansi za kimaumbile na za kiroho katika tafiti za kidini

Mwanazuoni huyu wa Hawza aliendelea kwa kurejea upana wa utafiti katika Uislamu akasema: Kila mwanafikra na mtafiti anapaswa kufikiri kuhusu masuala ya kimaumbile na kuinua sayansi za kimaumbile, na pia kwa upande wa kielimu na kifikra ashughulikie masuala ya kiroho. Kwa hivyo mhimili wa fikra na utafiti unapaswa kujumuisha pande zote mbili: masuala ya kimaumbile na vipengele vya kiroho na kifikra.

Maendeleo ya kweli yanategemea kuzingatia sayansi za kimaumbile kwa kuegemea misingi ya Qur’ani na kujiepusha na kuathiriwa na Magharibi

Marji' huyu wa Taqlidi, akirejea uzembe wa kihistoria wa Waislamu katika karne za mwanzo kuhusu dhana za kimaumbile katika Qur’ani, alibainisha: Maendeleo ya kweli ya kila jamii yanategemea kuzingatia maumbile na kuyatumia kwenye njia sahihi.

Mtukufu Ayatullah Subhani, akirejea aya za Qur’ani Tukufu zilizojaa ishara za matukio ya kimaumbile, alisema: Kwa masikitiko, Waislamu katika karne za mwanzo walizingatia kwa kiwango kidogo vipengele vya kimaumbile na kielimu vya aya za Qur’ani. Hali ya kuwa Qur’ani inazungumzia kwa upana masuala ya kimaumbile.

Tahadhari dhidi ya kuiga kipofu Magharibi na kusisitiza kujitegemea kifikra

Marji' huyu wa Taqlidi aliendelea kubainisha kuwa; sharti la msingi la maendeleo ni umakini wa kielimu na wa kimsingi, na akaonya kuwa: Ni lazima tuingie katika uwanja wa elimu kupitia njia sahihi, wala hatupaswi kuvutiwa na Magharibi. Sisi wenyewe tuna misingi sahihi ya kifikra. Ni lazima tuwe na uhuru wa kifikra na kielimu, na kuleweshwa na Magharibi hakupaswi kuathiri jamii.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha