Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kura za maoni miongoni mwa watu wa Palestina iliyokaliwa kimabavu, zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wakazi hao wanataka mateka wote waachiliwe huru, hata kama hilo litasababisha vita vya Israel dhidi ya Ghaza kufikia kikomo.
Hali kadhalika, Waziri wa Fedha wa serikali ya utawala haramu wa Kizayuni, kupitia tamko rasmi, alitangaza kuwa ana nia ya kuanzisha operesheni mpya ya kijeshi, na kwamba serikali ya utawala huo haina nia ya kukubali matakwa ya wananchi wake. Bezalel Smotrich alisema: "Mpango huu umepitishwa na baraza la mawaziri. Sisi Wazayuni tunaiita operesheni hii 'Utekaji wa Ghaza'."
Daima katika kipindi chote cha vita vya Ghaza, Smotrich, Netanyahu na wengineo, kwa misingi ya misimamo yao ya kibinafsi na ya kiuhuni, wamekuwa wakitaka kutumia vita kama “fursa ya kufufua tena vitongoji vya Kizayuni ndani ya Ukanda wa Ghaza” kwa maslahi yao binafsi.
Maoni yako