Jumamosi 27 Desemba 2025 - 16:00
Wosia wa Ayatullah al-‘Udhma Bashir Hussein Najafi kwa mwakilishi wa Mashia nchini Denmark

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Murid Hussein Naqvi alikutana na kufanya mazungumzo na Ayatullah al-‘Udhma Bashir Hussein Najafi hukk Najaf Ashraf.

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Murid Hussein Naqvi, mwakilishi wa Mashia wa Denmark, alikutana na kufanya mazungumzo na Ayatullah al-‘Udhma Haj Hafidh Bashir Hussein Najafi katika mji mtukufu wa Najaf Ashraf.

Katika mkutano huo, Ayatullah al-‘Udhma Bashir Hussein Najafi, akionesha furaha yake juu ya shughuli za kidini za Mashia wanaoishi barani Ulaya, hususan katika nchi za Skandinavia, aliulizia hali ya Waumini katika maeneo hayo na akazitaja juhudi zilizofanywa katika nyanja za kidini, kijamii na za tabligh kuwa ni za kupongezwa. Aidha, akisisitiza umuhimu wa nafasi ya wanazuoni na walinganiaji katika jamii za Magharibi, alitoa shukrani zake kwa huduma za thamani za Hujjatul-Islam Sayyid Murid Hussein Naqvi, na kumuombea mafanikio zaidi na kukubaliwa kwa huduma hizo mbele ya Mwenyezi Mungu.

Katika mwendelezo wa mkutano huo, pande zote mbili zilibadilishana mawazo kuhusu changamoto na masuala ya kidini na kijamii yanayowakabili Mashia wanaoishi Ulaya. Ayatullah al-‘Udhma Bashir Hussein Najafi, akirejea mazingira maalumu ya kitamaduni na kiakili ya jamii za Magharibi, alisisitiza ulazima wa kuhifadhi utambulisho wa kidini wa Mashia, kuimarisha misingi ya kiitikadi, na kutoa umuhimu maalumu kwa malezi ya kiakili na kimaadili ya kizazi kipya, sambamba na kuhitaji upangaji thabiti na wenye malengo katika nyanja hii.

Mkutano huo ulifanyika katika mazingira ya kirafiki na ya kiroho, na ndani yake kulisisitizwa umuhimu wa kuendeleza mawasiliano kati ya vituo vya kidini na jamii za Kishia zilizo nje ya nchi za Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha