Jumapili 28 Desemba 2025 - 21:00
Sheikh Khazali, azitaka taasisi za Kiislamu, Kiarabu na za kimataifa kutekeleza wajibu wao wa kibinadamu ili kusitisha mauaji nchini Syria

Hawza/ Katibu Mkuu wa Harakati ya Asaib Ahl al-Haq, amezitaka taasisi za Kiislamu, Kiarabu na za kimataifa kutekeleza wajibu wao wa kibinadamu ili kusitisha mauaji na ukiukwaji unaotishia maisha ya Wasyria.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Qais al-Khazali, Katibu Mkuu wa Harakati ya Asaib Ahl al-Haq, amezitaka taasisi za Kiislamu, Kiarabu na za kimataifa kutekeleza wajibu wao wa kibinadamu wa kusitisha mauaji na ukiukwaji unaotishia maisha ya wananchi wa Syria.

Sheikh Khazali amesema katika tamko lake kuwa; amepokea kwa “huzuni na masikitiko makubwa” habari ya shambulio la kujitoa mhanga la kikatili na lisilo la kiungwana, lililolenga waumini waliokuwa wakiswali Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Imamu Ali bin Abi Talib (amani iwe juu yake) katika mji wa Homs Syria, shambulio lililofanywa na mmoja wa wanachama wa makundi ya kitakfiri na kihalifu yanayojulikana kwa jina la “Ansar Ahl al-Sunna”, na kusababisha kuuawa kishahidi na kujeruhiwa kwa makumi ya raia wasio na hatia.

Aliongeza kusema: huku tukilaani na kukemea vikali kitendo hiki cha kinyama na cha woga, tunasisitiza juu ya umuhimu wa kuilinda jamii ya Syria, hasa makundi ya wachache, dhidi ya hatari na vitisho vinavyowafuatilia hadi katika nyumba zao, misikiti yao na shule zao.

Sheikh al-Khazali aliendelea kusema: tunazihimiza taasisi za Kiislamu, Kiarabu na za kimataifa kutekeleza wajibu wao wa kibinadamu wa kusitisha mauaji na ukiukwaji unaoyavuruga maisha ya Wasyria na kuhatarisha utulivu wa eneo zima.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha