Jumapili 28 Desemba 2025 - 19:00
Umoja wa Mataifa walaani mauwaji ya kiholela dhidi ya Mashia nchini Syria

Hawza/ António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amelaani vikali shambulio la kigaidi la hivi karibuni lililosababisha umwagaji damu, shambulio ambalo liliulenga Msikiti wa Imamu Ali (amani iwe juu yake) katika mji wa Homs, nchini Syria.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Stéphane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alitangaza kwamba, António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amelaani vikali shambulio la kigaidi la hivi karibuni lililo sababisha umwagaji damu, shambulio ambalo liliulenga Msikiti wa Imamu Ali (amani iwe juu yake) katika mji wa Homs nchini Syria.

Stéphane Dujarric alisema kuwa; Guterres analilaani kwa dhati shambulio hilo, na anasisitiza tena kwamba; mashambulizi dhidi ya raia na maeneo ya ibada hayakubaliki kabisa. Amehimiza umuhimu wa kuwatambua wahusika waliobeba dhamana ya shambulio hilo na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Katika kuendelea kwa tamko hilo, imeelezwa kuwa; Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatoa rambirambi zake za dhati kwa familia za waliouawa (mashahidi), anaeleza mshikamano wake na majeruhi wote, na anawaombea kupona wa haraka.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha