Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, hafla ya kupandishwa kwa bendera iliyoandikwa “Walid al-Ka‘bah” ilifanyika asubuhi ya leo, Jumapili (tarehe 8 Rajab 1447 Hijria, katika uwanja mtukufu wa Haidari wa Ataba Tukufu ya Alawi, chini ya kaulimbiu “عَلی حُبِّ علیّ” (Kwa mapenzi ya Ali). Hafla hii ni mwanzo wa programu za “Wiki ya Walid al-Ka‘bah” kuelekea maadhimisho ya kuzaliwa kwa heri kwa Amirul-Mu’minin Imamu Ali (amani iwe juu yake).
Katika hafla hiyo, Sayyid Issa al-Khurasan, Mkurugenzi Mkuu wa Ataba Tukufu ya Alawi, alihudhuria pamoja na naibu wake, wajumbe wa Baraza la Wadhamini, wakuu wa idara, kundi la wanazuoni, pamoja na watu mashuhuri wa kielimu na kijamii.
Uendeshaji wa hafla hiyo uliambatana na usomaji wa aya za Qur’ani Tukufu, hotuba iliyotelewa na Haidar al-Issawi, mjumbe wa Baraza la Wadhamini, iliyozungumzia mada ya kuhuisha ahadi na uaminifu, pamoja na uimbaji wa qaswida.
Kwa mujibu wa ripoti hii, “Wiki ya Walid al-Ka‘bah” inajumuisha mkusanyiko wa programu za kidini, kitamaduni na sherehe za wananchi; na katika kipindi hicho, miradi mingi ya huduma pia itazinduliwa katika mkoa wa Najaf Ashraf.



Maoni yako